DI MATEO ATUA UJERUMANI KUINOA SCHALKE 04
Kocha aliyeiongoza Chelsea kutwaa ubingwa wa kwanza wa klabu hiyo katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ROBERTO DI MATEO Ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani
Di Mateo ambaye amekua 'mtaani' bila kazi Tangu Novemba mwaka 2012 miezi michache baada ya kuwapa Chelsea Ubingwa wa Ulaya na kombe la FA.
DI Mateo amejiunga na Schalke 04 kuchukua nafasi ya kocha aliyetimuliwa Jens Keller ambaye ametimuliwa baada ya kucheza mechi 10 msimu huu huku akipata ushindi mara 2 tu kocha ambaye amedumu na Schalke mwezi Novemba 2012.
Mtihani mkubwa kwa Di Mateo ni tarehe 25 mwezi huu atakapowakaribisha Chelsea katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Taarifa iliyotolewa mkurugenzi wa Michezo wa Schalke 04 Horst Heldt kwa waandishi wa habari ilisema "Lengo la kubadilisha kocha ni kupata changamoto mpya na tunaamini kuwa Di Mateo ni mtu sahihi wa kuifanya kazi hiyo. Schalke wanakamata nafasi ya 11 hivi sasa katika msimamo wa ligi ya Ujerumani.
Di Mateo amekua nje ya soka tangu alipotimuliwa Chelsea mwaka 2012 na taarifa zilizopo zinasema tangu Novemba mwaka huo alipotimuliwa Di Mateo amekua akilipwa mshahara wake wa paundi 130,000 kila wiki mpaka mwezi June mwaka huu ambapo mkataba wake ulikua umeisha.
××××××××××××××××××××××××××××××÷÷

No comments