HABARI 8 KALI ZA SOKA LEO JUMAPILI


             ■■    NYUMBANI


1. Timu ya Taifa ya Tanzania imeibuka na ushindi mnono wa bao 4-1 dhidi ya Benin katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Magoli ya Stars yakifungwa na Canavaro,Kiemba,Ulimwengu na Luizio



2. Kocha wa Toto Afrika John Tegete amemtambia Kocha wa Mwadui Jamhuri Kiwelu Julio kuwa hamuwezi baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya timu yake wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara.

3. Mwamuzi Israel Nkongo ndiye atachezesha pambano la watani wa jadi Simba na Yanga Jumamosi ijayo katika uwanja wa Taifa Dar ikiwa ni mechi za nne kwa timu hizo katika mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Simba iko Afrika Kusini na kuna taarifa kuwa Yanga imejichimbia Zanzibar.

     ■ ■AFRIKA NA ULAYA


4. Michael Essien amekanusha taarifa zilizozagaa katika mitandao mbalimbali kama ameambukizwa Ugonjwa wa Ebola na kusema habari hizo ni za uzushi kwani yeye yuko salama akiwa na klabu yake ya AC Milan.

5. Goli pekee la Wayne Rooney liliipa ushindi mwembamba England katika mechi dhidi ya Estonia ugenini na kuwafanya vijana hao wa Roy Hudgson kuongoza kundi E wakiwa na pointi 9 baada ya michezo miatatu.

6. Diego Costa amefunga goli lake la kwanza kwa Timu ya Taifa ya Spain katika mchezo wa kuwania kuchsza fainali za mataifa ya Ulaya. Spain wakishinda kwa bao 4-0 dhidi ya Luxembourg.

7. Bayern Munich wameweka mezani kiasi cha paundi milion 30 kumnasa kiungo mshambuliaji wa Arsenal na Timu ya taifa ya Ujerumani Mesuit Ozil na inawezekana January akatimkia Uerumani.

8. Manchester United pengine wanaweza sasa kumsajili Artudo Vidal lakini itawalazimu kumwachia Juan Mata ambaye Juventus wanamtaka.

... Usisahau ku like ukurasa wetu Facebook (Wapenda Soka- kandanda)

×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.