WENGER AMUOMBA MSAMAHA MOURINHO KIAINA



Si kawaida mara nyingi kwa mkubwa kuomba msamha pale anapokosea lakini Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ameibuka na kuomba msamaha kufuatia kitendo chake cha kumsukumua kocha wa Chelsea Jose Mourinho katika pambano baina ya timu hizo katika dimba la Stamford Bridge maarufu kama Darajani.

Katika mchezo huo ambao Wenger na kikosi chake walikubali kichapo cha bao 2-0 kulitokea purukushana baina ya makocha hao wawili ambapo Wenger alimsukuma Mourinho baada ya Beki wa Chelsea Gary Cahil kumfanyia madhambi Alexis Sanchez wa Arsenal.



Mourinho anadai alikua akimzuia Wenger kuingia katika eneo la ufundi la Chelsea ila Wenger anasema Mourinho alimsema vibaya na yeye akahamaki na kufanya alichofanya.

"Najuatia kwa kilichotokea na naomba radhi kwa tukio hilo halikua tukio la kufurahisha katika uwanja wa soka japo vyombo vya habari vimelipamba sana.
Najua hali ya mchezo mara nyingi hupelekea watu kupaniki lakini haikua vizuri kufanya vile" alisema Wenger.

Katika siku za karibuni Makocha hao wawili ambao timu zao ziko mji mmoja wamekua wakipamba sana habari za Soka kwa kurushiana maneno ya hapa na pale na Wenger ameshindwa kuomba msamaha kwa Morinho moja kwa moja.

Ushindi walioupata Chelsea wa bao 2-0 dhidi ya Arsenal si tu umewaweka kileleni na kuwafanya timu pekee ambayo haijafungwa mchezo wowote msimu huu lakini pia umeongeza Uteja kwa Kocha Arsene Wenger dhidi ya Jose Mourinho kwani hakuna mchezo ambao Wenger ameshinda dhidi ya Mourinho licha ya kucheza michezo 12 mpaka sasa.

××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.