WAKALI WAPYA WATATU NDANI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA MSIMU HUU
Ule usiku uliokua unasubiriwa kwa hamu kubwa na mamilioni ya wapenzi wa soka Duniani sasa umewadia.Viwanja 8 kuwaka moto wakati miamba 16 kutoka nchi mbalimbali barani Ulaya zikitoana jasho.Wakati Dunia ikiwa na hamu ya kuwaona nyota kama Lionel Messi,Ronaldo,Ibrahimovic,Robben na wengine wengi,Jicho langu litakua makini kuwatazama nyota wapya wanaotarajiwa kuiteka michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu.
Ligi ya mabingwa Ulaya inarudi katika jiji la Liverpool klabu yenye historia kubwa ya michuano hiyo baada ya kutoshiriki kwa miaka mitano.
Pia itakua michuano yenye kuleta machungu kwa mashabiki wa Manchester United kwani watakua wanashuhudia tu klabu zingine baada ya kushindwa kupata nafasi ya kushiriki kutokana na matokeo mabovu ya msimu uliopita.
Wapo nyota wengi wanaotarajiwa kucheza michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa mara ya kwanza ,lakini jicho langu litakua linawaangalia kwa karibu hawa wafuatao.
RAHEEM STERLING
Kocha Rafael Benitez wa Liverpool atakua karibu na Tv yake akitathmini kazi ya ubongo wake uliomleta Raheem Sterling Liverpool kutoka QPR mwaka 2010. Nyota ya Raheem Sterling iling’aa zaidi msimu uliopita ambapo ndani ya msimu huo nyota huyo alipachika jumla ya mabao 11 kati ya hayo 9 yakiwa katika ligi kuu na mawili katika kombe la Fa. Raheem Sterling anatarajia kucheza mechi ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya hii leo dhidi ya Ludogorets kutoka Bulgaria.
Baada ya kuondoka kwa Luis Suarez,Sterling ameachiwa mzigo wa kuhakikisha Liverpool inapata matokeo kwenye mazingira ya aina yeyote. Kasi na akili ni silaha kubwa ya Raheem Sterling.Mipango ya ushindi kwa Liverpool na hata timu ya Taifa ya England inaanzia kwenye miguu ya Raheem sterling.
Kocha Brendan Rogers alimpumzisha katika mechi dhidi ya Aston Vila ili kumweka sawa na mechi hii
CIRO IMMOBILE
Alianza Mohamed Zidan akaja Lucas Barrios mpaka kwa Robert Lewandowski na sasa ni Ciro Immobile. Msimu uliopita mchezaji huyo wa zamani wa Torino ya Italia aliibuka kidedea na kushinda “Capocannoniere” baada ya kupachika mabao 22.
Mpaka sasa hajaifungia Borrusia Dortmund lakini nyota huyo anatarajiwa kutakata kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya ambapo atacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Arsenal leo jioni kwenye uwanja wa Signal iduna ambao ni uwanja wa nyumbani wa Dortmund. Nyota huyo ambaye miguu yake ni rafiki wa karibu na nyavu atashirikiana kwa karibu na Adrian Ramos na Aubameyang kuendeleza kile alichokua akikifanya Lewandowski.
MUNIR EL HADDADI.
Hawa ndio Barcelona,Nani alishawai kumzungumzia mchezaji huyu kabla ya msimu huu mpya?. Sifa ziwaendee wakatalunya hawa wanaojua kusafisha nyota za wachezaji chipukizi. Wakati Luis Suarez akiendelea kutumikia adhabu yake, Chipukizi Munir El haddadi anaendelea kuuthibitishia uma kuwa La masia hawabahatishi.Kinda huyo raia wa Spain mwenye Asili ya Morocco mpaka sasa ameshiriki kwenye michezo yote 3 ya Barcelona na kupachika bao moja.
Wiki iliyopita kwa mara ya kwanza munir el haddadi alicheza kwenye timu ya taifa ya spain dhidi ya Macedonia kwenye mchezo wa kusaka tiketi katika michuano ya ulaya 2016.Wengi wanabashiri kuwa Munir ndie mchezaji atakayevaa viatu vya lionel Messi.Munir anatarajiwa kukipiga kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Apoel Nicosia kwenye uwanja wa camp nou siku ya jumatano.
■■ RATIBA KAMILI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Leo Jumanne
21:45 Olympiakos Piraeus vs Atlético Madrid
21:45 Juventus vs Malmö FF
21:45 Liverpool vs Ludogorets
21:45 Real Madrid vs Basel
21:45 Monaco vs Bayer Leverkusen
21:45 Benfica vs Zenit
21:45 Galatasaray vs Anderlecht
21:45 Borussia Dortmund vs Arsenal
Kesho Jumatano
21:45 Roma vs CSKA Moskva
21:45 Bayern München vs Manchester City
21:45 Barcelona vs APOEL
21:45 Ajax vs PSG
21:45 Chelsea vs Schalke 04
21:45 Maribor vs Sporting CP
21:45 Porto vs BATE
21:45 Athletic Club vs Shakhtar Donetsk
Na Allen Kaijage
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments