ANELKA AJIUNGA NA MUMBAY CITY YA INDIA
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Nicolas Anelka amejiunga na klabu ya Mumbai City inayoshiriki ligi kuu nchini India maarufu kama Indian Super League (ISL)
Anelka mwenye miaka 35 alikua hana timu tangu alipoondoka West Brom kufatia utovu wa nidhamu.
Anelka ambaye ameichezea Ufaransa mara 69 alianza kuchza soka akiwa na PSG kabla hajajiunga na Arsenal. Badae akachezea Real Madrid,Manchester City,Fenerbahce, Bolton, Chelsea, Shanghai Shenhua, Juventus na West Brom na kumfanya kufikisha klabu yake ya 11 tangu alipoanza kusakata kabumbu.
Anelka anaenda India katika mkakati uliowekwa na Wahindi kuboresha Ligi yao ya Soka baada ya kupotea katika ramani ya Soka na ataungana na wachezaji wengine wa zamani wa Arsenal akiwemo Freddie Ljungberg, Alessandro Del Piero na David Trezeguet ambao tayari wanakipiga katika Ligi hiyo.
Msimu mpya wa Ligi ya India utaanza mwezi Oktoba ambao utakua msimu mfupi ambao utadumu mpaka mwezi Disemba.
{ Edo DC}
No comments