BAADA YA MIEZI MITANO NJE BENTEKE AKARIBIA KURUDI ASTON VILLA



Mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke anatarajia kurudi dimbani siku za karibuni baada ya kuanza mazoezi na kikosi cha timu ya kwanza.
Benteke mwenye miaka 23 alikua nje ya uwanja tangu April mwaka huu alipoumia na kupelekea kukosa fainali za kombe la Dunia kule Brazil.

Mwenyewe ame"tweet" katika akaunti yake ya twita akisema kuwa "Miezi mitano sasa, Ilikua safari ndefu lakini nafurahi kwani kurudi tena uwanjani kufanya kitu ninachokipenda kuliko vyote.
Asanteni kwa Ushirikiano mlionipa mbarikiwe sana"



Benteke ilibidi apatiwe matibabu maalumu chini ya daktari wake binafsi Lieven Maesschalk ambaye amemsaidia na kuweza kurudi uwanjani wakati huu ambapo Aston Villa wanakabiliwa na michezo migumu katika ligi ikiwa ni pamoja na Mchezo wa Tarehe 20 dhidi ya Arsenal nyumbani kabla hawajaenda ugenini kucheza na Chelsea tarehe 27.
Badae watacheza na Man City Nyumbani Octoba 4 kabla hawajaenda Goodson Park kukutana na Everton

Kwa taarifa yako tu Aston Villa inakamata nafsi ya Pili katika msimamo wa ligi hivi sasa ikiwa ndo timu pekee ambayo imefungwa magoli machache ikiwa imefungwa goli moja tu na kufunga magoli manne,na ni kati ya timu tatu ambazo hazijafungwa tangu ligi ianze ikiungana na Arsenal na Chelsea ambazo nazo hazijafungwa.

{Edo Dan Chibo}


No comments

Powered by Blogger.