ARSENAL HOFU TUPU : DEBUCHY "NJE" MIEZI MIWILI
Klabu ya Arsenal huenda ikazikosa huduma za mlinzi wake wa kulia Mfaransa Mathieu Debuchy kwa muda wa miezi miwili au zaidi
kufuatia maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mchezo wa ligi kuu dhidi
ya Manchester City uliopigwa katika dimba la Emirates.
Debuchy alitolewa nje kwa machela dakika ya 81 ya mchezo kufuatia kujikwaa na kuangua wakati akijaribu kumiliki mpira kulikopelekea
kuumia kwa kifundo cha mguu wake wa kushoto.Vipimo vya awali vimeonyesha kuwa mlinzi huyo hajavunjika kama ilivyodhaniwa na badala yake vinasubiriwa vipimo vingine (scanning) ili kubaini ukubwa wa jeraha na muda wa matibabu ambao unahisiwa utakuwa kati ya miezi miwili mpaka mitatu.
Kufuatia kuumia kwa Debuchy,Arsenal inabaki na walinzi watano wanaopaswa
kuziba nafasi tano zilizoko katika idara hiyo huku kinda Calum Chambers akichukua
jukumu la kucheza nafai ya ulinzi wa kulia katika mchezo wa jumanne wa ligi ya mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund.
Debuchy mbali ya kuukosa mchezo dhidi ya Dortmund pia atakozikosa mechi kadhaa za ligi zikiwemo dhidi ya Spurs na Chelsea pamoja na Galatasaray na Anderletch kwenye ligi ya mabingwa Ulaya.
Akizungumzia hilo kocha Wenger alisema “Hakuna mvunjiko wowote alioupata lakini ni jeraha kubwa.Ni baya na siyo zuri hata kidogo.
~Paul Manjale (Wapenda Soka group)
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++××++++×××+××+××××
No comments