TAARIFA KAMILI YA MECHI YA AZAM FC NA POLISI MOROGORO
Na Allen Kaijage - Chamazi Complex
Timu ya Azam fc imeanza vyema harakati zake za kutetea taji la ligi kuu bara kwa kuichapa timu ya polisi morogoro bao 3- 1. Shukrani zimuendee Didier Kavumbagu aliyefunga magoli mawili ,moja katika kila kipindi.
Goli la kwanza la Azam lilifungwa dakika 14 ya na mshambuliaji Didier kavumbagu baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kipre tchetche,Haikuishia hapo dakika 8 mbele Kipre tchetche alipiga mpira wa adhabu uliokutana moja kwa moja na kichwa cha Agrey morice na kutumbukia wavuni.Mpaka kipindi cha pili kinaisha Azam walikua mbele kwa mabao hayo mawili.Katika kipindi Hiko cha kwanza dakika ya 30 kocha Rishard alifanya mabadiliko kwa kumtoa Bantu Admin na Kumuingiza James Mganda.
Kipindi chote cha kwanza Azam walitawala mchezo huo huku wachezaji Kipre Balou na Kiungo chipukizi Mudathir Yahya wakitawala vyema safu ya kiungo.Kipre Tchetche aliwasumbua sana mabeki wa Polisi Morogoro sambamba na kumjaribu kipa Tony Kavishe kwa mashuti kazaa.Washambuliaji wa timu ya Polisi Dany Mrwanda na Salum Machaku hawakufurukuta mbele ya beki ya Azam iliyokua inaongozwa na Agrey Morice na David Mwantika.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu lakini ilikua polisi Morogoro iliyopata bao lake pekee kwenye mechi hiyo dakika ya 60 baada ya Machaku kumuanzishia mpira wa kona Nahoda Bakari aliyetupia moja kwa moja wavuni.Kocha wa Polisi morogoro aliwatoa Nahoda Bakari na kuingia Edgar Charles na Nicholous Kabope akapumzika na kuingia Selembe.Mabadiliko hayo yalileta chachu kwenye timu ya polisi morogoro.Dakika ya 72 almanusura polisi morogoro wasawazishe goli baada ya Machaku kupiga Shuti kali lililogonga mwamba.Ila Yule Yule aliyeianza kazi Didier Kavumbagu akamaliza kazi kwa kupachika goli la 3 kwa Azam baada ya mabeki wa polisi kushindwa kuokoa mpira wa kona ndani ya eneo la hatari.
MTAZAMO WA MWANDISHI
Kwa nilivyoiona mechi hiyo Polisi Morogoro wanakazi kubwa ya kufanya ili kujihakikishia nafasi ya kubaki ligi kuu.Salum Machaku ndie mchezaji pekee wa polisi aliyekuwa na madhara kwa Azam kwa kupiga mashuti 4 yaliyolenga goli.Wachezaji wengi wa polisi wanaonekana si wazoefu wa ligi kuu jambo ambalo linaweza kuwagharimu maafande hao.
Kwa upande wa Azam wana kazi ya ziada kama wanataka kweli kufika mbali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika.Mpaka dakika ya 50 pumzi za viungo wa azam zilikua zimekata jambo ambalo liliwapa mwanya polisi morogoro kupanga vyema mashambulizi yao.

No comments