... KARIBU KATIKA SHOW YA DI MARIA LEO ....
Kama ilivyo ada leo wale mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Uingereza, Manchester united watakuwa katika dimba la ugenini Uwanja wa King Power kupambana na Leicester City timu ambayo imepanda daraja msimu huu.
Tusitarajie mechi rahisi kwa hawa mashetani kwa sababu Leicester City wanacheza ki ari kubwa sana na imani ya kuondoka hata na pointi hasa wakiwa katika dimba la nyumbani... Mechi mbili zilizopita wamefanikiwa kupata point nne sawa na Manchester united.
Upande wa united, ambayo imeanza kucheza soka la kuvutia kidogo kutokana na pass zao wanazopiga na wanavyojitahidi kumiliki mpira, hasa katika nafasi ya kiungo ambayo inatawaliwa na fundi wa kidutch asiyeonekana Daley blind pamoja na muispaniola Ander herrera.
Jicho kubwa leo litakuwa kwa mchezaji ghali wa ligi hiyo, Angel Di Maria. Si jambo geni ukicheza game ya FIFA kusikia mpira ukiguswa na Jack Wilshere au Magician Messi yule commentator akisema hili neno "he is a natural dribbler".
Ndivyo ilivyo kwa huyu jamaa wa kiargentina. Ana sura ya kipole sana lakini ana miguu ya kikatili, ana uwezo wa kukimbia dakika tisini bila kuchoka, na ana uwezo wa kulazimisha mabeki kufanya kile anachokitaka yeye kisha akapiga pasi murua ambayo hufika pale anapotaka yeye.. Kiwango chake cha upigaji pasi pale ligi nzima hakuna wa kulinganisha naye zaidi ya Mesut Ozil wa arsenal na Cesc Fabregas wa chelsea. Hawa ndio wapo katika daraja moja la upigaji pasi.
Katika mchezo iliopita Di Maria alikua mwiba mchungu kwa ngome ya QPR akishiriki katika magoli yote manne.
Man United inaingia katika mchezo wa leo macho ya mashabiki yakiwa kwa kijana huyu aliyenunuliwa na Manchester United akitokea Real Madrid. Magoli na pasi za mwisho zinategemewa kutoka katika miguu ya huyu jamaa.
Uwanja wa King Power utakaotumika kwa mchezo wa leo |
Mfumo ambao huenda kocha wa Man United atautumia leo ni 4-1-2-1-2 ambao ambao aliutumia katika mchezo uliopita mfumo ambao una wachezaji wengi kama anavyotaka yeye mwenyewe. Naona kama leo Louis atampa nafasi Mcolombia Falcao kuanza kama namba tisa na nahodha Wayne Rooney akianza kama namba kumi.... Japokua anaweza kuwachezesha wote watatu yani Rooney,Van Perse na Falcao kama alivyofanya kipindi cha pili katika mchezo uliopita.
Kikosi kamili kinachotabiriwa kwa upande wa Manchester united leo ni kama kifuatacho;
De gea
Rafa evanc rojo shaw
Blind
Herrera di maria
Mata
Falcao rooney.
Hapa mfumo wa Almasi ( diamond formation) unaonekana kupendeza kwa sababu inaruhusu wachezaji wote isipokuwa namba sita na kipa kupishana nafasi wakati wakicheza hivyo kuwachanganya wapinzani. Hata hivyo kama nilivyosema awali kuwa Leicester City si ya kuibeza hasa ikiwa nyumbani kwao, ila kwa uwepo wa Di Maria, Rooney, Blind, Rojo, Falcao tutegemee mechi nzuri yenye ushindani ambayo haitakuwa na sare.
Utabiri wangu ni
Leicester City 1-3 Man United
Tukutane saa tisa na nusu.
{By; Sylvaction Rojo Maria toka Wapenda Soka group katika facebook}
..... note: Kwa mshabiki wa timu yoyote ambaye ungependa tuirushe habari yako tutumie kwa Whatsapp 0762427272 au email. wapendasoka@gmail.com
No comments