KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : MTAZAMO WA MECHI ZA LEO KATIKA SOKA



Karibu tena katika kijiwe cha Wapenda Soka Leo tukiangalia baadhi ya michezo itakayopigwa leo huku Wapenda Soka wakijaribu kutoa maoni na mitazamo yao kuhusu mechi za leo

VPL - TANZANIA
4:30 PM  Simba SC vs Coastal Union

CHRISS COACHER
" Hawa ni ndugu wawili wanaocheza mpira wa pasi  nyingi mno ..huku SIMBA ikiwa chini ya mzambia Patrick Phiri haitashangaza kuona wakiibugiza Coastal Union mabao ya kutosha kutokana na uwezo wa mzambia huyu kufundisha.

Phiri ameonekana kujaribu kutatua tatizo kubwa la SIMBA idara ya beki wa kati japokua kesi inaweza kuwa tofauti kwani Wagosi wa kaya wana (Coastal Union) wana wachezaji wenye uwezo mkubwa na mara nyingi wamekua wakiisumbua Simba wanapokutana.
Lakini kukosekana kwa udhamini uliokuwepo hapo kabla wa Binslum unaweza pia kuwashusha morali Coastal Union.

Natarajia pambano lenye ladha na lenye kuvutia katika Ligi Kuu Tanzania Bara na sio pambano la kulikosa"

UTABIRI WANGU
SIMBA 3 -2 COASTAL UNION



Barclays Premier League

Leicester City vs Manchester United (saa tisa na nusu)

JUMA MKILINDI
"Kwa haraka haraka wawezasema hii game ni ya Mancherster A vs Machester B
Kwani karibia wachezaji 8 wote wa Leicester city walipitia Manchester utd, huku watano wakiwa kiwa kwa mkopo

Ktk wachezaji hao 8 watatu ambao ni
Ritchie de laet
Danny Drinkwater
Na Matty James
Hawa watacheza, lakini wachezaji watano ambao ni

Tom Lawrence
Danny Simposon
Jack Barmby
Louis Rowley
Nick Powell

Hawa watazuiliwa na sheria ya Mkopo kwa kutokucheza dhidi ya tm yao halisi.

Record ya Matokeo
Manchester utd imeshinda mechi 9 mfululizo kabla ya mchezaji wa Leicester cty kuja kuvunja record hio mwaka 1998 january ambapo Leicester walishinda kwa 1-0,goal la Tony Cottee pale OT

Ktk uwanja wa King Power, Leicester waliweka record ya kushinda mechi 17 kati ya 23 za Championship
Mara ya mwisho kushinda ktk ligi kuu ilikua mwaka 2004 dhidi ya Portsmouth,

Huku Manchester wakitegemea nyota wao wapya kama Herrera,Rojo,Falcao,Blind na Dimaria ambao wamegharim kiasi cha ppaundi 150 mill,

Leicester cty wanamtegemea zaidi mchezaji wao ambae amevunja record ya Club kwa usajili uliogharim paund 8 mill,
Muagentina Lonardo Ulloa ambae amefunga goli 3 kati ya michezo mi4 alocheza.
Akisaidiwa na kiungo Matty James na kipa Kasper Schmichel ambao wanarudi kutokana na walikua majeruhi.

Kutokana na Recoerd hizi mechi itakua rahisi kwa utd ila wasitegemee mtelemko

MAN CITY vs CHELSEA. (saa 12 jioni)

PATRICK ABSALOM
"Hii ndio mechi kubwa City akiwa mwenyeji wa Chelsea (Etihad stadium)  kwenye mzunguko wa Tano Ligi Kuu Uingereza. Ikizikutanisha timu ambazo zinapewa nafasi kubwa kutwaa UBINGWA mwishoni.

  Chelsea wataingia mchezoni wakiwa na 100% baada ya kushinda michezo yote minne. Wakionyesha kukamilika kila Idara akiwemo mshambuliaji wao hatari Diego Costa akiwa kwenye kiwango cha hali ya juu, City itakuwa kipimo tosha kwao msimu huu.

  Manchester city wameonyesha kutanga tanga wakitafuta makali waliyo maliza nayo msimu ulioisha baada ya kufungwa na Stoke City na mchezo uliofuatia kugawana pointi Na Arsenal ugenini. City wataingia kwenye mchezo huu dhamira ikiwa ni kupunguza gepu la pointi 5 na kulipiza kisasi cha msimu uliopita walipopoteza nyumbani na ugenini.

Natazamia mchezo kuwa mzuri na wa kuvutia, usikose kuwa mbele ya runinga kushuhudia mechi hii.

UTABIRI WANGU;
CITY  3-1 CHELSEA"

Spanish Primera División

Levante vs Barcelona
EDO DANIEL CHIBO
Mechi nyingine ambayo huwezi kutabiri matokeo yake kwani mara nyingi Levante wanawapa Tabu Barcelona hapa nategemea mechi nzuri sana kuiangalia jioni hii.

UTABIRI WANGU

Levante 2-2 Barcelona

Kwa leo ni haya tu.

No comments

Powered by Blogger.