RONALDO NA MESSI: YUPI ATAIPIKU MAPEMA REKODI YA RAUL LIGI YA MABINGWA ULAYA?
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana alifunga goli la 3 katika ushindi wa bao 5-1 walioupata mabingwa watetezi Real Madrid dhidi ya FC Basel katika Ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya Makundi katika Kundi B ambalo pia lina timu za Liverpool na Ludogorets.
Ronaldo ambaye pia ni. Mchezaji bora wa mashindano hayo mwaka jana alifunga goli lake la 68 katika historia ya michuano hiyo likiwa goli moja zaidi ya magoli aliyofunga Lionel Messi ambaye ameshafunga magoli 67.
Rekodi ya mchezaji aliyefunga magoli mengi katika ligi ya mabingwa Ulaya inashikiliwa na Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Raul Gonzales ambaye amefunga magoli 71 rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa na watu pekee wanaoonekana kuikaribia ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Wakati Ronaldo amebakiza magoli matatu kufikia rekodi hiyo,Messi anadaiwa magoli manne kufikia rekodi hiyo huku macho ya WAPENDA SOKA leo tukisubiri kuangalia atafanya nini Messi katika mechi yao ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Apoel Nicosia.
Kwa Mtazamo wako unadhani yupi kati yao atawahi kufikia au kuvunja rekodi hiyo?
RATIBA YA MECHI ZA LEO JUMATANO - LIGI YA MABINGWA ULAYA.
21:45 Roma vs CSKA Moskva
21:45 Bayern München vs Manchester City
21:45 Barcelona vs APOEL
21:45 Ajax vs PSG
21:45 Chelsea vs Schalke 04
21:45 Maribor vs Sporting CP
21:45 Porto vs BATE
21:45 Athletic Club vs Shakhtar Donetsk
{Na Edo Daniel Chibo }
No comments