KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : TATHMINI YA MECHI BAYERN MUNICH vs MAN CITY 


Usiku wa Ulaya unaendelea tena leo kwa Mechi 8 kupigwa katika viwanja 8 tofauti huku miamba ya Soka Barani Ulaya ikijaribu bahati zao za kushinda mechi za awali katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Baada ya Jana Jumanne kushuhudia michezo ya makundi A mpaka D ikipigwa leo itakua mechi za makundi manne yaliyobaki yani kuanzia kundi E mpaka Kundi H.

Katika KIJIWE CHA WAPENDA SOKA leo tunaumulika mchezo wa kundi E kati ya Bayern Munich na Manchester City mchezo utakaopigwa katika dimba la Alianz Arena Jijini Munich Ujerumani.

Ni mechi ambayo inazikutanisha timu ambazo msimu uljopita zilikua katika kundi Moja Kundi D katika michuano hii na Bayern Munich Kumaliza juu ya Kundi ikifatiwa na Manchester City nafasi iliyoipelekea Man City kukumbana na Barcelona katika hatua ya 16 ambapo ndiyo ilikua mwisho wao.

Kijiweni leo tunautazama mchezo huu kama ndo mchezo uliobeba siku ya leo huku tukitarajia vibanda umiza kujaza mno kutokana na timu zote mbili kua na vikosi timilifu kila idara.
Na baadhi ya Wapenda Soka walitoa mawazo yao kama ifuatavyo:-



BAB CHICHARITO

"Majeruhi yanaweza kuigharimu Bayern Munich kwani watawakosa wachezaji wao muhimu lakini kama wakiwa makini na kuwashambulia City vizuri kuna kila sababu ya kuamini Bayern Wataibuka na ushindi leo.
Man City kwa upande wao wapo vizuri na wamejiandaa na mashindano haya kuna kitu wanataka kuprove kwa watu na hata mabosi wao kama wamekomaa sasa katika michuano hii na hicho ndo kinatufanya Wapenda Soka tutamani kuangalia hii Mechi.
Utabiri wangu unaenda kwa Man City na nawapa ushindi.
Bayern Munich 1-2 Manchester City"

EDO DANIEL CHIBO

" Kwanza tukiangalia kwa haraka Bayern Munich wanaweza wakawakosa Frank Ribbery na Arjen Robben wanaosumbuliwa na maumivu ya goti japokua ripoti ya daktari inasubiriwa kuona kama watacheza.

Lakini Schweinsteiger, Thiago Alcantara,Rafinha na Javi Martinez hawa ni majeruhi wa muda mrefu hawawezi kurudi mapema japokua namwona Xabi Alonso akiingia moja kwa moja katika kikosi cha Bayern Munich na pengine ataanza leo ikiwa ni mechi yake ya kwanza akiwa na Bayern Munich katika ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya usajili wa paundi milioni 5 toka Real Madrid.

Kwa Upande wa Man City majeruhi waliopo kikosini ni Stevan Jovetic na Fernando ambao wanasumbuliwa na misuli ya paja.
Zabaleta anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa mwisho msimu uliopita dhidi ya Barcelona hivyo Bakary Sagna anaweza kuanza nafasi hiyo.
Kocha Manuel Pellegrin pia atakosa mchezo huu baada ya kufungiwa kufuatia utovu wa nidhamu hivyo kocha msaidi Ruben Cousillas atakua na jukumu la kuwaongoza mabingwa hao wa England dhidi ya mabingwa wa Ujerumani.

Yaya Toure atarudi baada ya kukosa mechi dhidi ya Arsenal akimaliza ule muungano ulioleta mafanikio makubwa msimu uliopita akiwa na Fernandinho jambo ambalo linanipa matumaini makubwa sana ya kuamini kua Man City atashinda leo kama alivyofanya msimu uliopita.

Wakati Bayern Munich wanamtegemea Mueller na Lewandowski City wao wana Aguero na Dzeko. City wana pia Silva,Nasri,Navas na Toure ambao pia ni warahisi kufunga.
Utabiri wangu unamwangukia Man City japo naamini shughuli itakua pevu.
FC Bayern Munich 2-3 Manchester City"

UTABIRI MWINGINE WA WAPENDA SOKA.

ADRIAN DANIEL
Bayern Munich 2-2 Man City

ALLY MGAZZAH
Bayern Munich 2-1 Man City

SALV TESHA
Bayern Munich 4-1 Man City

 RATIBA YA MECHI ZA LEO JUMATANO - LIGI YA MABINGWA ULAYA.

KUNDI E
21:45 Roma vs CSKA Moskva
21:45 Bayern München vs Manchester City

 KUNDI F
21:45 Barcelona vs APOEL
21:45 Ajax vs PSG

KUNDI G
21:45 Chelsea vs Schalke 04
21:45 Maribor vs Sporting CP

KUNDI H
21:45 FC Porto vs BATE
21:45 Athletic Bilbao vs Shakhtar Donetsk

Asanteni na tukutane muda mwingine.
Usisahau kulike page ya wapenda soka (wapenda soka-kandanda) katika ukurasa wa Facebook.


No comments

Powered by Blogger.