LIGI YA MABINGWA ULAYA - TIMU ZA ENGLAND HOI.

Fabregas akishangilia goli

Mechi za kwanza za hatua ya makundi ligi ya mabingwa Ulaya zilimalizika jana kwa timu za England kuendelea kufanya vibaya.

Chelsea ikiwa nyumbani Darajani ililazimishwa sare na Schalke 04 ya Ujerumani. Chelsea wakitangulia kufunga kupitia kwa Cesc Fabregas dakika ya 11 tu ya mchezo kabla ya Schalke hawajasawazisha dakika 62 kwa goli safi kabisa la Klaas Huntelaar na kufanya mchezo huo wa kundi G kumalizika kwa sare ya 1-1.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu England Manchester City licha ya kuwamudu vyema Bayern Munich walijikuta wakifungwa goli dakika ya 90 ya mchezo kupitia kwa Jerome Boateng baada ya mabeki wa City kushindwa kuokoa mpira wa kona.

Kwa matokeo hayo Liverpool ndo timu pekee toka Katika ligi kuu England Iliyopata  ushindi katika mchezo wake wa Awali baada ya kuwafunga PFC Ludogorets ya Bulgaria bao 2-1 mchezo uliopigwa Jumanne ktika dimba la Enfield kwa magoli ya Mario Balotel na Steven Gerard.
Arsenal wao walikubali kichapo cha bao 2-0 ugenini wakicheza na Borussia Dortmund.



Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitaendelea tena baada ya wiki mbili na haya ndo matokeo yote ya jana Usiku pamoja na Wafungaji:-

KUNDI E

Roma 5-1 CSKA Moskva
{ Iturbe 6',Gervinho 10',31' ,Maicon 20', Ignashevich (og) 50'}
( Ahmed Musa 82')

Bayern München 1-0 Manchester City
{ Boateng 90' }

 KUNDI F
Barcelona 1-0 APOEL
{ Pique 28'}

Ajax 1-1 PSG
{Cavan 14, Schoene 74'}

KUNDI G
Chelsea 1-1 Schalke 04
{ Fabregas 11', Huntelaar 62'}

Maribor 1-1 Sporting CP
{ Luis Nani 80' , Zahovic 90'}

KUNDI H
FC Porto 6-0 BATE
{Brahimi Brahimi 5',32' 57' Martinez 37', Adrian 61', Aboubakar 76'}

Athletic Bilbao 0-0 Shakhtar Donetsk

{Na Edo Daniel Chibo }

No comments

Powered by Blogger.