KWA TAARIFA YAKO - MAMBO MUHIMU USIYOYAJUA KUHUSU LIGI YA MABINGWA ULAYA
MJUE
MTUNZI WA WIMBO WA LIGI YA MABINGWA
Habari na Paul Manjale
Tony
Britten:Huyu ndiye mtunzi wa wimbo maarufu
wa ligi ya mabingwa Ulaya.Wimbo huo ambao uko katika lugha za Kiingereza,Kifaransa
na Kijerumani ulitungwa mwaka
1992 wakati wa kuanzishwa kwa mfumo mpya wa michuano hii ambao tuko nao mpaka
sasa.Britten hakutunga wimbo huo kwa ajili ya kujifurahisha yeye bali ilikuwa
ni matakwa ya chama cha soka barani Ulaya kuwa na wimbo wake ambao
utatambulisha michuano hiyo.Wimbo huo umeimbwa na waimbaji wa Academy of St.Martin iliyoko Uingereza.
JE,
JOAO BAPTISTA MARTINS NI NANI?
Huyu ndiye mfungaji wa goli la
kwanza la michuano hii mwaka 1955
ilipoanza rasmi ilikuwa ni katika mchezo wa hatua ya makundi kati ya Sporting
Lisbon na Partizan Belgrade katika mchezo ulioisha kwa vilabu hivyo kutoka sare
ya goli 3-3.Baptista alikuwa akiichezea Sporting wakati huo,huku ubingwa wa
kwanza ukitwaliwa na klabu ya Real
Madrid baada ya kuibamiza klabu ya Reims
kwa goli 4-3.Shukrani kwa magoli ya
Alfredo Di Stefano,Narquiton na Hector
Rial aliyefunga mara mbili.Baptista alifunga goli hilo dakika ya 14 ya
mchezo huo ulipigwa Sept 4 jijini Lisbon katika dimba la Nacional.
Francisco
"Paco" Gento López
Ni mshindi mara sita wa taji hili
aliwa na klabu ya Real Madrid miaka 1956, 1957, 1958, 1959, 1960 na 1966.
KIKOMBE
Kombe la ligi ya mabingwa lina urefu wa sentimeta 74 na limetengenezwa
kwa shaba mwaka 1967,lina uzito wa kilo 11.Lilitengenezwa na Jorg Stadelmann sonara toka Bern,Uswisi
kwa gharama ya pesa za Kiswisi 10,000 (Swiss Francs).Hili ni kombe la
pili baada ya lile la awali kutwaliwa moja kwa moja na klabu ya Real Madrid
mwaka 1966 kama heshima ya kulinyakua mara ya sita.
Timu yoyote ambayo hutwaa taji hilo
mara tatu mfululizo ama mara tano kwa ujumla wake hupewa heshima ya kulitwaa
kombe hilo moja kwa moja.Timu ambazo zimepata heshima hiyo ni Real Madrid,Ajax, Bayern Munich,Ac Milan na
Liverpool.
Pamoja na kikombe pia hutolewa jumla
ya medali 40 za dhahabu kwa mshindi huku mshindi wa pili nae huvuna jumla ya
medali 40 za fedha.(Hii ni kuanzia mwaka 2012 mpaka sasa).
Kikosi cha Real Madrid ambacho kilitwaa ubingwa wa kwanza wa
Ulaya
|
JE,MALIPO
YAKOJE?
Kama waswahili wasemavyo kazi na
dawa basi ndivyo ilivyo hata katika michuano hii ambapo kila hatua timu shiriki kujikusanyia
kitita fulani cha pesa.Mchanganuo uko kama ifuatavyo nah ii ni katika Euros.
·
Mtoano:2,100,000
·
Makundi: 8,600,000
·
Ushindi(Kila mchezo hatua ya
makundi): 1,000,000
·
Sare(Mchezo wa makundi): 500,000
·
Hatua ya 16 bora: 3,500,000
·
Robo fainali: 3,900,000
·
Nusu fainali: 4,900,000
·
Mshindi wa pili: 6,500,000
·
Bingwa: 10,500,000
WADHAMINI:
Michuano hii ina jumla ya wadhamini
wanane wakuu ambao ni Master Card,Sony,Playstation,Nissan,Gazprom,Heineken,UniCredit
na HTC pamoja na Adidas na Konami’s Pro Evolution Soccer kama wadhamini wadogo daraja la pili.
JE, ADIDAS
NI NANI KATIKA MICHUANO HII?
Adidas mbali ya kuwa ni moja kati ya
wadhamini wakubwa wa michuano hii pia ndiyo
kampuni pekee yenye haki ya kutengeneza mipira na jezi za waamuzi wote wanaochezesha
michuano hii.
JE,HEINEKEN NI NANI?
Heineken hawa ni wadhamini wakubwa zaidi kuliko
AdidasKampuni hii ya kutengeneza pombe ndiyo iliyochukua nafasi kubwa zaidi
katika michuano hii.Ila kama ilivyokawaida katika jambo lolote lile changamoto
huwa hazikosi sasa sikia hii.
Heineken ni marufuku katika nchi za Ufaransa,Kazakhstan,Urusi,Uturuki na
Slovenia,udhamini wa pombe michezoni hauruhusiwi katika nchi hizo.Hivyo
katika nchi za Ufaransa,Uswisi na baadhi ya maeneo ya Hispania nafasi ya
Heineken huchukuliwa na “Enjoy Responsibly”
ama “Open your world”.Katika nchi za Urusi,Uturuki na Kazakhstan,udhamini
huwa mikononi mwa Respect.
VIPI UMRI WA WAAMUZI?
Tangu mwaka 1990 waamuzi wa michuano
hii hawapaswi kuwa na umri unaozidi miaka 45.Mwamuzi
akifikisha umri huo huachia ngazi hata kama alikuwa bora kiasi gani.Kigezo
hicho kimewekwa ili kuhakikisha waamuzi wote wanakuwa vizuri kiafya.
TUNAKARIBISHA MAONI KWA AJILI YA
KUBORESHA BLOG HII JISIKIE HURU KUONGEA CHOCHOTE KILE CHENYE
KUJENGA.......ASANTENI!!
No comments