ARSENAL NA ATLETICO MADRID ZAANZA NA VICHAPO ULAYA.


Usiku wa mabingwa Ulaya ulianza vibaya kwa Mabingwa wa La Liga klabu ya Atletico Madrid baada ya kuchapwa bao 3-2 na Olympiakos ya Ugiriki pambano la kundi A lililopigwa katika dimba la Olympiakos.

Magoli ya Wagiriki hao yalifungwa na Masuaku,Affelay na Mitroglou wakati Atletico Madrid walipata magoli yao kupitia kwa Mandzukic na Griezman.

Mechi nyingine ya kundi A ilishuhudia Juventus ikiibamiza Malmo bao 2-0 magoli yote yakiwekwa kimiani na Carlos Tevez.

Arsenal wakisafiri mpaka jiji la Dortmund Ujerumani walijikuta wakibamizwa bao 2-0 na Borussia Dortmund magoli yote mawili yakifungwa kwa wastani wa dakika chache na Immobile na Aubameyang na kuwafanya vijana wa Wenger kupoteza mechi yao ya kwanza katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.



Ligi ya Mabingwa ilirudi katika jiji la Liverpool kwa Ushindi wa bao 2-1 walioupata Wenyeji Liverpool dhidi ya timu ngeni ya Ludogorets.

Mabingwa watetezi Real Madrid walitoa kipigo cha bao 5-1 wakiwafunga FC Basel ya Uswis katika pambano kali lililipigwa katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid

MATOKEO KAMILI YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA USIKU:

KUNDI A
Olympiakos Piraeus 3-2 Atlético Madrid
{Masuaku 13,Affelay 31' na Mitroglou 74'}
{Mandzukic 38', Griezman 87'}

Juventus 2-0 Malmö FF
{Carlos Tevez 59', 90'}

KUNDI B
Liverpool 2-1 Ludogorets
{Mario Ballotel 82',Gerard 90'}
(Dani Abalo 90')

Real Madrid 5-1 Basel
{Marek Suchy (OG) 14' Gareth Bale 30', Ronaldo 31' James 37', Benzema 79'}
(Derlis Gonzalez 38')

KUNDI C
Monaco 1-0 Bayer Leverkusen
{Joao Mortinho 61'}

Benfica 0-2 Zenit
{Hulk 5', Witsel 22'}

KUNDI D
Galatasaray 1-1 Anderlecht
{ Dennis Praet 52'}
{ Burak Yilmaz 90'}

Borussia Dortmund 2-0 Arsenal
{ Ciro Immobile 45', Aubameyang 48'}

RATIBA YA MECHI ZA LEO - JUMATANO

21:45 Roma vs CSKA Moskva
21:45 Bayern München vs Manchester City
21:45 Barcelona vs APOEL
21:45 Ajax vs PSG
21:45 Chelsea vs Schalke 04
21:45 Maribor vs Sporting CP
21:45 Porto vs BATE
21:45 Athletic Club vs Shakhtar Donetsk

{Na Edo Daniel Chibo }

No comments

Powered by Blogger.