KUELEKEA KATIKA MCHEZO DHIDI YA ARSENAL JUMAMOSI- HII NDIYO ASTON VILLA



Kuelekea mchezo wa Jumamosi hii dhidi ya Arsenal Klabu ya Aston Villa imeendelea na maandalizi yake kukabiliana na ratiba ngumu ya Ligi ambayo iko mbele yao. Hii ndo timu pekee ambayo Ratiba yake inaonekana ngumu katika ligi.

Wakiwa katika kiwango bora kabisa tangu kuanza kwa Ligi wakikamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi nyuma ya Chelsea na pia ikiwa ni kati ya timu tatu ambazo hazijafungwa mpaka sasa wanaingia katika mchezo mwingine mgumu baada ya kupata ushindi ugenini dhidi ya Liverpool hii ni katika mfululizo wa mwezi wenye mechi ngumu zaidi kwani baada ya Arsenal nyumbani itasafiri kuwafata Chelsea Ugenini badae watawaalika Man City.

MAANDALIZI YAKOJE KWA VILLA?



Kuelekea mechi hiyo na zingine zijazo Villa inaendelea kufanya maandalizi wakati huu ambapo inakamata nafasi ya Pili hivi sasa baada ya mechi 4 tangu ligi kuanza ikiwa ni mara ya kwanza baada ya  miaka 16 mara ya mwisho ilikua msimu wa mwaka 1998/1999 ambapo mpaka kufikia Christmas Aston Villa ilikua ikiongoza ligi japokua ilikuja kuteleza mechi za mwisho na kuishia nafasi ya 6 mwisho wa Ligi.
Hii inanipa sababu ya kuamini kuwa huu pia unaweza kua msimu mzuri kwa Villa hasa kwa kuangalia ubora wa kikosi cha sasa na jinsi vijana wa Lambert alioanza kuwanoa miaka miwili iliyopita wakizoeana na kucheza kitimu zaidi

 Katika kusuport kile kinachofanyika klabuni Uongozi wa klabu umeamua Kumwongezea mkataba kocha Paul Lambert ambapo sasa atakaa Villa Park kama kocha mpaka June 2018 baada ya kusaini kufundisha Aston Villa June mwaka 2012.

Benchi la Ufundi limeimarishwa pia kutokana na ujio wa Mchezaji wa Zamani wa Man United Roy Keane ambaye amejiunga na klabu hiyo kama kocha msaidizi mwanzoni mwa msimu.

Usajili makini uliofanywa na Benchi la Ufundi la Villa kwa kuwaongeza kiungo Mkolombia Carlos Sanchez, Winga wa zamani wa Chelsea Joe Cole,mlinzi wa zamani wa Arsenal Philipe Senderos pamoja na kiungo mshambuliaji TOM CLEVERLEY Ambaye amejiunga na Villa kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester United hawa wamekuja kuwaimarisha vijana waliopo klabuni.

Mshambuliaji Christian Benteke aliyekua majeruhi ameanza mazoezi mepesi pamoja na kikosi cha kwanza haijajulikana bado kama Kocha Paul Lambert anaweza kumpanga ila Gabriel Agbonlahor ambaye aliwaua majogoo wa jiji ataendelea kucheza pale mbele akisaidiana na Weimann huku dimba la Juu akichezesha Tom Cleverley na Delph.

Je ASTON VILLA Wataifunga Arsenal kama walivyofanya msimu uliopita? TUSUBIRI DAKIKA 90.

Endelea kuwaalika marafiki ku like page ya Wapenda Soka - Kandanda katika mtandao wa Facebook.

{ Edo Daniel Chibo}

No comments

Powered by Blogger.