LIGI KUU TANZANIA BARA - YANGA WAKO MORO LEO SIMBA WANAANZIA TAIFA KESHO.
Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League inaanza leo kwa viwanja Sita kuwa katika wakati mgumu huku timu 12 kati ya 14 zinazoshiriki ligi hiyo zikijitupa uwanjani.
Mabingwa watetezi Azam FC wao wataanzia Nyumbani Chamazi Complex kuvaana na timu ngeni ya Polisi Morogoro mchezo ambao pengine unaweza kupigwa majira ya Usiku baada ya ukarabati wa uwanja huo kukamilika ikiwa ni pamoja na kuwekwa taa za kuwezesha mechi kucheza Usiku.
Makamu Bingwa Yanga SC itasafiri kuwavaa Mtibwa Sugar ya Morogoro pambano litakalopigwa katika uwanja wa Jamuhuri majira ya saa 10 jioni.
Ni pambano ambalo litawakutanisha kocha wa zamani wa Tanzania Marcio Maximo ambaye anainoa Yanga hivi sasa na Beki wa zamani wa Tanzania Mecky Maxime ambaye ni kocha mkuu wa Mtibwa Sugar.
Washindi wa Tatu Msimu uliopita klabu ya Mbeya City wao watakua Nyumbani Sokoine Pale jijini Mbeya kuwakaribisha JKT Ruvu.
Simba wao wataanza kampeni yao wakiwa na Kocha mpya Patrick Phiri kesho Jumapili kwa kuumana na Coastal Union katika mchezo utakaopigwa Katika dimba la Taifa kuanzia saa 10 jioni.
Wageni wa Ligi Ndanda FC ya Mtwara iko tayari Shinyanga kuwavaa wageni wengine wa Ligi Stendi United ya mkoani Shinyanga.
Ruvu Shooting wao watakua uwanja wa mabatini pale Kibaha kuwavaa Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Mgambo JKT ya Tanga itakua uwanja wa Mkwakwani kuwaalika Kagera Sugar toka Kagera.
RATIBA KAMILI
Azam FC vs Polisi Morogoro
Mtibwa Sugar vs Yanga SC
Mbeya City vs JKT Ruvu
Mgambo vs Kagera Sugar
Stendi United vs Ndanda FC
Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons
... Usisahau kulike page ya Wapenda soka katika mtandao wa facebook (wapenda soka - kandanda)
+++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments