LIGI KUU ENGLAND ~ LIVERPOOL YABAMIZWA 3-1 NA MAN CITY.
![]() |
Jovetic |
... Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Manchester City Wameipiga bila huruma makamu bingwa Liverpool kwa bao 3-1 katika pambano la ligi kuu ya England lililopigwa katika dimba la Etihad jijini Manchester.
Man City walianza kuhesabu karamu ya magoli dakika ya 41 kupitia kwa mshambuliaji wake Stevan Jovetic na kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili Man City waliendelea kuinyanyasa safu ya ulinzi ya Liverpool kwa magoli ya Stevan Jovetic dakika ya 55 huku Sergio Kun Aguero akifunga bao zuri sekunde chache baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Edin Dzeko dakika ya 69.
Goli la Liverpool lilitokana na makosa ya beki wa Man City Pablo Zabaleta dakika ya 83 nafasi iliyowapa Liverpool goli baada mlinzi huyo kujifunga.
Licha ya kufungwa Liverpool pia ilipata piga baada ya wachezaji wake Glen Johnson na Moreno kuumia.
MATUKIO MUHIMU
- Yaya Toure dakika ya 29 na Emre Can dakika ya 76 ndiyo waliopata kadi za njano.
- Man City walipiga mashuti manne yaliyolenga goli la Liverpool wakati Liverpool wao walipiga mashuti matatu.
- Liverpool walipata kona 7 wakati Man City walipata kona 6.
- Man City walicheza faulo mara 13 wakati Liverpool wao walicheza faulo 7.
- Umiliki wa mpira ulikua 50% - 50% kwa timu zote.
++++++++++++++++++++++++++++++
No comments