The Gunning Machine ~ FABREGAS ANAKATA JONGOO KWA MENO
"Hata
Yesu Kristo angechezea Arsenal, kuna siku angeondoka tu. Fabregas kitu gani
bwana".
Haya yalikua ni maneno ya rafiki yangu mmoja anaitwa Charles siku moja hivi mwaka 2011.
Hiyo ilikua ni baada ya mimi kumwonyesha picha ya nahodha wake kipenzi Cesc Fabregas akitambulishwa huko Catalunya Nyumbani kwa Barcelona.
Sikushangazwa sana na maneno yake kwa sababu kati ya mashabiki jeuri kabisa duniani ni mashabiki wa Arsenal. Mashabiki wa Arsenal huwa hawana tabu. Hawaoni shida kuchoma moto jezi za wachezaji wanaowasaliti.
Charles hakua na cha kujali. Angejali nini wakati hata Patrick Vieira aliwahi kuondoka na akaishia kufulia huko Juventus? Alichobaki kufanya Charles ni kumwombea mabaya Fabregas.
Binafsi kama shabiki wa Arsenal niliumia sana kumpoteza Cesc. Hii ni kwa sababu Cesc ni aina ya Wachezaji ninaowapenda sana. Cesc alishaotesha mizizi yake moyoni mwangu. Lakini haikua na jinsi, nikalazimika kuwa kama Charles, nikamtukana Arsene Wenger lile tusi letu maarufu mjini, maisha yakasonga. Nikakata jongoo kwa meno.
Arsenal ilihangaika sana kuziba pengo lake, hasa baada ya kutimka kwa Samir Nasri kuelekea Manchester City.
Haya yalikua ni maneno ya rafiki yangu mmoja anaitwa Charles siku moja hivi mwaka 2011.
Hiyo ilikua ni baada ya mimi kumwonyesha picha ya nahodha wake kipenzi Cesc Fabregas akitambulishwa huko Catalunya Nyumbani kwa Barcelona.
Sikushangazwa sana na maneno yake kwa sababu kati ya mashabiki jeuri kabisa duniani ni mashabiki wa Arsenal. Mashabiki wa Arsenal huwa hawana tabu. Hawaoni shida kuchoma moto jezi za wachezaji wanaowasaliti.
Charles hakua na cha kujali. Angejali nini wakati hata Patrick Vieira aliwahi kuondoka na akaishia kufulia huko Juventus? Alichobaki kufanya Charles ni kumwombea mabaya Fabregas.
Binafsi kama shabiki wa Arsenal niliumia sana kumpoteza Cesc. Hii ni kwa sababu Cesc ni aina ya Wachezaji ninaowapenda sana. Cesc alishaotesha mizizi yake moyoni mwangu. Lakini haikua na jinsi, nikalazimika kuwa kama Charles, nikamtukana Arsene Wenger lile tusi letu maarufu mjini, maisha yakasonga. Nikakata jongoo kwa meno.
Arsenal ilihangaika sana kuziba pengo lake, hasa baada ya kutimka kwa Samir Nasri kuelekea Manchester City.

Alikuaja Mikel Arteta lakini bado hakua Fabregas. Maisha yalikua magumu mno bila Cesc, kila mtu aliona. Hii ni kwa sababu tayari timu ilishajengwa kupitia yeye.
Ili kuondoa mzimu wa Fabregas ilibidi Arsenal iundwe upya kwa kumzunguka mtu mwingine ambaye ni mshambuliaji Robin Van Persie ndio kidogo Fabregas akaanza kufutika mioyoni mwa mashabiki wa Arsenal.
Kuna mtu anaitwa Mbwiga wa Mbwiguke. Ana msemo wake maarufu sana anasema, "Mungu si Mzee Mkumba". Sijui mzee Mkumba ni nani lakini matukio mengi ya kuudhi katika maisha hulipwa hapa apa duniani.
Sikushangaa sana nilipowasikia washabiki wa Barcelona wakimzomea Cesc katika mchezo dhidi ya Athletic Bilbao . Sikushangaa kwa sababu najua kwamba Barcelona hawaijui thamani yake. Hawakumzomea kwa sababu ya kucheza chini ya kiwango, hata Messi huwa anashuka kiwango lakini hawawezi kumzomea.
Walimzomea kwa sababu alijirahisisha sana kwao. Alijikosesha thamani mbele yao.
Cesc aliihitaji Barcelona kuliko Barcelona ilivomhitaji yeye, ndio maana alikua tayari kulipa kiasi cha £1m kila mwaka kutoka kwenye mshahara wake kwa kipindi cha miaka mitano ili
kukamilisha ada yake ya uhamisho kutoka Arsenal.
Timu inayokuhitaji haikununui kwa mtindo huu hata siku moja. Ni sawa na
mwanamke kumlazimisha mwanaume amwoe tena kwa kujilipia mahari wakati mwanaume
alikua na uwezo wa kulipa lakini hakutaka. Mwanamke huyu hawezi kuheshimiwa na
mumewe kamwe.
Ndicho kilichomkuta Cesc.Maisha yalimbadilikia pale Catalunya hasa baada ya kuondoka kwa kocha wake Pep Guadiola, sasa imefikia hatua ni lazima aondoke kwa sababu hahitajiki tena.
Cesc anaondoka Barcelona miezi michache tu baada ya kutamka kwa kinywa chake kwamba aliumbwa kuchezea klabu mbili tu duniani ambazo ni Barcelona na Arsenal.
"Nina furaha sana hapa, hakuna mpango wowote wa mimi kuondoka. Nilikuja hapa nikitokea Arsenal ambako nilithaminiwa hivyo siamini kama naweza kucheza kwingine "
Hayo ni maneno ya Cesc baada ya tetesi kumhusisha na Man utd mwaka 2013.
Arsenal ndio klabu iliyopewa kipaumbele katika biashara ya Fabregas na hata yeye alikua tayari kurejea Emirates lakini bahati mbaya sana kwake ni kwamba Arsene Wenger hakumuhitaji tena Cesc.
Kumrejesha Cesc ni aina ya biashara ambayo Wenger asingeweza kuifanya
kwa wakati huu Kwa sababu amekwisha toa kiasi kikubwa cha pesa kumnunua Mesut Ozil
ambae anatoa huduma inayofanana na ile ya Fabregas.
Lakini pia anao vijana ambao kimsingi wanastahili nafasi ambazo wamezipigania kwa kipindi kirefu. Hawa si wengine, ni Aaron Ramsey na Jack Wilshere. Hawa wanachukuliwa kama Arsenal damu na wapo kwenye mioyo ya washabiki wa Arsenal. Wamehangaika sana na viwango vyao hawa vijana.
Aaron Ramsey amewahi kuzomewa mara kadhaa tena katika uwanja wake wa nyumbani wa Emirates kutokana na kiwango kibovu lakini hakukata tamaa wala hakuwaza kuhama mpaka sasa amekua mchezaji kamili.
Kumrudisha Cesc, ambaye pamoja na thamani kubwa aliyopewa pale Arsenal bado aliamua kuondoka zake ni kumsaliti Ramsey ambaye amefanikiwa kutoka kuwa mchezaji anayechukiwa zaidi mpaka kuwa mchezaji tegemeo. Ingewakatisha tamaa wachezaji wa aina hii.
Lakini pia Arsenal haina upungufu kwenye safu ya ya kiungo kwa sasa. Inao Santi Cazorla, Thomas Rosicky, Wilshere na Ramsey na kumwongeza mwingine wa Gharama kubwa ni kutupa pesa.
Sasa Fabregas amekwenda Chaelsea. Ameamua kumtafuna jongoo kwa meno yake. Inataka moyo sana. Kwa nini nasema hivi.
Cesc akiwa Arsenal aliuaminisha ulimwengu kwamba yeye ni Arsenal, na alikua Arsenal kwelikweli. Alikua na tabia za mashabiki wa Arsenal kabisa. Alikua anaichukia Chelsea, aliwahi kumpiga Alex Ferguson na Pizza pale Old Traford, na aliwahi kutoa matamshi ya kejeli sana juu ya timu nyingine.
Sasa katika timu ambazo haikuwahi kufikirika kama Fabregas anaweza kucheza ni Chelsea.
Chelsea ni wapinzani wenye nguvu kwa Arsenal. Wanafundishwa na kocha ambae huwatia kichefuchefu sana washabiki jeuri wa Arsenal.
Baada ya habari kutangazwa rasmi juzi kuhusu Cesc kujiunga na Chelsea, kuliibuka maswali mengi sana karibu toka pande zote za dunia watu wakihoji kwanini Fabregas anakwenda Chelsea klabu ambayo mara kadhaa amenukuliwa akisema anaichukia kuliko vitu vyote?Wapo waliokwenda mbali zaidi hata kufikia hatua ya kuchoma moto jezi zake na kumtakia mabaya huko aendako.Mashabiki wa klabu yake ya zamani ya Arsenal wamepost picha mitandaoni zikiwaonyesha wakichoma jezi za klabu hiyo zenye no 4 mgongoni ambazo zilivaliwa na kiungo huyo enzi akichezea klabu hiyo.
Kama kuchoma jezi ni njia au ishara ya kumlaani Fabregas basi mashabiki wa Arsenal wanapaswa kujua wameilaani pia klabu yao pendwa..
Kama kuna klabu ambayo ilipewa nafasi ya kwanza kumsajili Fabregas ni Arsenal tena kwa masharti mepesi na rahisi iliyoweka yeyenye miaka mitatu iliyopita.Walichotakiwa kufanya hapa Arsenal ni kuwaambia Barcelona ``We want our boy back home" na Barcelona wangeitikia ``Yes!!fast like a wind" na mchezo ungeishia hapo.
Lakini Arsenal tena kupitia kocha wake mkuu Arsene Wenger wamekuwa mstali wa mbele kumkana kijana huyu aliyeonyesha kila dalili za kutaka kurudi Emirates.Walichokuwa wakikiwinda Arsenal ni ile fidia yao ya £5m ambayo wangeipata kutokana na mauzo ya nyota huyo kwenda klabu yoyote ile.
TULITAKA AENDE WAPI??
The Gunning Machine Inaamini kuwa Fabregas hakuwa na jinsi. Arsenal hawakumtaka, Real Madrid hawawezzi kumtaka, Bayern Munich hawakumtaka,Man City imekamilika, Man Utd haipo Champions League na yeye alishataka kurudi England.
Timu pekee ya saizi yake iliyomtaka ni Chelsea na ndiko angalau unapoweza kupata pesa na vikombe.
Ila kwa kwenda Chelsea ni sawa na kujitangazia vita ya moja kwa moja na mashabiki wa
Arsenal. Ni lazima wamzomee hata kama atakua hashangilii akiwafunga, ndivo walivo. Ni bora ushangilie tu kama alivofanya Robin Van Persie.
Kwenda Chelsea kwa Fabregas ni sawa na kumkata jongoo kwa meno, ni ujasiri wa hali ya juu.
...... Imeandaliwa na Richard Leonce Chardboy (WS)
TUKUTANE JUMAMOSI IJAYO KATIKA THE GUNNING MACHINE NYINGINE
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


No comments