KOMBE LA DUNIA ~ KIPIGO CHA MPWA MWIZI KIMEIPATA SPAIN NA KULIZA WATU MITAANI BONGO
![]() |
| RVP akifunga moja ya magoli bora kabisa |
Unaweza ukarudi kulala ukidhani kama Hukumalizia usingizi na ndicho kilichotokea Usiku huu ambapo Spain mabingwa watetezi wamejikuta wakiangukia pua baada ya kufungwa bao 5-1 na Uholanzi katika mechi ya kwanza ya kundi B katika fainali ya Kombe la Dunia pale Brazil mechi iliyopigwa katika dimba la Fonte Nova.
![]() |
| Alonso akifunga Penati |
Kipigo hicho kwa Spain kimekuja baada ya miaka 41 walipopata kipigo cha goli nyingi namna hii. Ilikua miaka 41 iliyopita yani mwaka 1963 ambapo Spain walifungwa na Scotland bao 6-2 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Mchezo huu ulikua ni kama Marudio ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 kule South Africa ambapo Spain waliibuka Kidedea.
HALI YA MITAA YA BONGO
Jicho letu mtaani Bongo lilishuhudia matokeo hayo yakileta hisia tofauti lakini hasa yakiliza watu wengi hasa wale wanaopenda Kubet kwani wengi wao walitabiri kuwa Spain atashinda au mchezo utaisha kwa sare na kuweka pesa nyingi sana kwa Mhindi (Msimamizi wa michezo ya kubashiri).
Kwa Upande mwingine ilikua shangwe sana kwa Mashabiki wa Man United ambao wamependezwa na jinsi vile timu ya kocha wao mpya ilivyokua ikicheza huku mshambuliaji wa Timu hiyo Robin Van Perse akifanya mambo makubwa.
Katika Mechi Nyingine iliyotangulia ilishuhudia mechi ya kundi A kati ya Mexico na Cameroon, Mexico wakichomoza na ushindi mwembamba wa bao 1-0 goli la dakika ya 61 la mshambuliaji Oribe Peralta.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


No comments