KOMBE LA DUNIA ~ VIOJA VYA RONALDINHO FEKI NA REKODI MPYA ZAWEKWA WAKATI BRAZIL IKISHINDA 3-1.
Fainali za Kombe la dunia mwaka huu Zimeanza jana Usiku kwa sherehe kubwa za Ufunguzi katika jiji la Sao Paulo Nchini Brazil ambapo maelfu ya mashabiki wa duniani walilipamba jiji hilo kwa Bendera mbali mbali lakini hasa zile za Njano na kijana za wenyeji Brazil.
Mechi ya Ufunguzi Ilishuhudiwa na Mashabiki 65,000 walioingia Uwanjani huku ikikadiriwa kutazamwa na Watu zaidi ya Bilion moja Duniani kote.
Katika mechi ya Ufunguzi Jana Usiku Wenyeji Brazil waliifunga timu ya Taifa ya Croatia Goli 3-1 goli 2 za Neymar na Moja la Oscar huku Marcelo akitangulia kujifunga goli lililowapa uongozi Wageni Croatia.
REKODI ZILIZOWEKWA
- Goli la Kwanza Kabisa katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazili lilifungwa dakika ya 11 likiwa ni goli la kujifunga la beki wa kushoto wa Brazil Hilo ndo goli la kwanza katika historia ya Fainal za kombe la Dunia kuwahi kujifunga na mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil.
- Mchezo wa Jana ulikua ni mchezo wa 98 kwa timu ya Taifa ya Brazil Tangu waanze kushiriki Fainali za Kombe la Dunia wakishinda mechi 68 kati ya hizo.
- Neymar alifunga magoli mawili jana ambayo yamemfanya kufikisha Magoli 33 katika mechi yake ya 50 kuichezea timu ya Taifa ya Brazil.
- Ushindi wa goli 3-1 walioupata Brazil umeifanya timu hiyo kufikisha Jumla ya Magoli 214 katika michezo yao 98.
Katika Mchezo wa Jana Kioja kikubwa kilikua maamuzi ya Refa Mjapanikuizawadia Brazil Penati ambayo ilizua utata.
Nishimura alipiga kipenga na kuashiria penalti baada ya Dejan Lovren kuonekana kama aliyemtega Fred katika eneo la lango, hata hivyo picha za runinga zilizorejelea mara kadhaa hazikuonesha kama Lovren alimgusa Fred.
Wachezaji wa Croatia walijaribu kumshawishi mjapan huyo kuwa haikuwa kweli Fred alikuwa amejiangusha lakini maoni yao hayakusikika.
KIOJA CHA RONALDINHO FEKI
Kabla ya Mchezo huo kulitokea pia Kituko kikubwa katika mazoezi ya timu ya Taifa ya Argentina
Katika hali isiyokuwa ya kawaida nyota wa soka duniani Lionel Messi amejikuta akikaribishwa Brazil kwa style ya pekee.
Messi ambaye alikuwa akifanya mazoezi na kikosi cha timu yake ya taifa katika uwanja wao Estadio Independencia alijikuta katika mshangao mkubwa baada ya kushindwa kumtambua Ronaldinho feki aliyekuja kumsabahi.
Ronaldinho huyo feki anaitwa Robinson Oliveira ambaye inasemekana amefanana sana nyota wa soka wa Brazil Ronaldinho Gaucho.Oliveira ambaye amekuwa akiwachanganya wengi kutokana na kufanana huko na nyota huyo alikuwa miongoni mwa maelfu ya mashabiki wa soka walioruka uzio na kuvamia uwanja kwa ajili ya kuona na japo kuwagusa nyota wa Argentina hasa Messi.
Messi baada ya kumuona Ronaldinho feki hakutambua kama aliyeko mbele yake ni Robinson Oliveira na siyo Ronaldinho kama akili yake ilivyomtuma.
Messi akasema "Hukupaswa kuja mbio kunifuata kama walivyofanya mashabiki hawa wewe ni kaka yangu ungeita tuu Messi nami ningekufuata"
Messi hakujua kuwa yule siyo Ronaldinho anayemjua bali ni Robinson Oliveira mtu anayeishi mjini kutokana tuu na kufanana na Ronaldinho Gaucho.
Baada ya Messi kugundua hilo alionekana kustaajabu na kuangua bonge ya kicheko cha mwaka.Kituko kingine kilikuwa ni shabiki mmoja aliyekuja akainana na kuanza kuishangaa miguu ya Messi akitaka kujua nini kilichomo katika miguu hiyo hata iwe hatari zaidi dimbani.
MWEZI MZIMA WA REKODI NA VITUKO MBALI MBALI UTAVIPATA HAPA HAPA KWA WAPENDA SOKA BLOG. BLOG NAMBA MOJA AMBAYO HAIKOPI HABARI TOKA KATIKA BLOG ZINGINE
Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo na Paul Manjale (Members wa Wapenda Soka Group)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++



Na rekodi nyingine ni kuwa Marcelo amekuwa mchezaji wa kwanza wa Brazil kuwahi kujifunga katika world cup.
ReplyDelete