KWA TAARIFA YAKO ~ MWANAMAMA HUYU NDO MMILIKI WA SOUTHAMPTON
Katharina Liebherr:
Jina hili la mama huyu kibonge si maarafu sana katika vichwa na midomo ya wapenda soka duniani hasa bongo,labda ni kwa sababu ya jinsia yake ama ni kutokana na tabia yake ya kujiweka mbali na vyombo vya habari.
Katharina ni binti wa marehemu billionea Marcus Liebherr aliyefariki mwaka 2010 kwa ugonjwa wa moyo (heart attack) ambapo mwaka mmoja nyuma yaani 2009 billionea huyu alitoa Paundi milion 14 tuu kuinunua klabu machachari ya Southampton iliyokuwa katika harakati za kujikwamua kufilisika.
Klabu ya Southampton ndiyo klabu ambayo ina mchango mkubwa katika uanzishwaji wa vilabu viwili maarufu vya Hispania. Klabu hii ndiyo iliyokuwa ikiviuzia jezi vilabu vya Atletico Bilbao na majirani zao Atletico Madrid miaka ile ya 1889-1950.
Klabu hii ndiyo iliyomkuza na kumuibua nyota ghali zaidi duniani kwa sasa Gareth Bale wa Real Madrid pamoja na "mapacha" wawili Theo Walcott na Alex Oxlade Chamberlain wa Arsenal
Je,Katharina ni nani hasa mpaka nimzungumzie??

Huyu ndiye bosi wa akina Victor Wanyama,Adam Lallana,Luke Shaw na Morgan Schneiderlain kwa lugha nyepesi na rahisi zaidi huyu ndiye mmiliki wa klabu ya Southampton ya England Klabu inayosifika kuibua vipaji.
Huwezi kumpata Shaw ama Lallana bila ya mama huyu kuridhia,mama huyu anamwita mmiliki wa Chelsea jina lake la kwanza yaani Roman na jamaa hachukii.Kiti anachokalia mama huyu, Wenger na Mourinho hawakalii....pesa IPO!!Vijana wake kibao wako Brazil kwenye mshikemshike wa kombe la dunia .....Upo?
Basi Kwa Taarifa yako katika orodha ya wamiliki wa vilabu vya Ligi Kuu England ongeza na jina la huyu mwanamama wa kiswiss kama Ulikua hujaliweka au ulikua ukibababika Kujua mmiliki wa Southampton.
.....Imeandaliwa na Paul Manjale (WS)
Note: usiikose makala Hii ya Kwa taarifa Yako kila Jumatano na Jumapili hapa hapa Katika Wapenda Soka blog.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments