HAZARD AIKANA PSG AKOMAA NA CHELSEA NA KUSISITIZA HAHAMI
Winga wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard amesisitiza kuwa hafikirii kuihama klabu hiyo ya Darajani.
Hazard aliyesajililwa Chelsea June mwaka 2012 kwa ada ya uhamisho wa Paundi milion 32 amefunga magoli 17 msimu ulioipita alikua akihojiwa na Gazeti la Le Derniere Heure la Ubelgiji alinukuliwa akisema "Uhakika wa kubaki Chelsea ni 100% klabu imenithamini ndiyo maana ikataka kufanya nami mazungumzo juu ya Mkataba mpya
PSG hawajawahi kunifata hivyo swala la mimi kuhamia PSG ni uzushi"
Katika wiki za karibuni Hazard ambaye amepewa jezi namba 10 iliyokua ikivaliwa na Juan Mata aliyetimukia Man United, amekua akihusishwa kwa kiwango kikubwa kuhamia katika klabu ya PSG ya Ufaransa.
Kwasasa Hazard yuko Brazil na kikosi cha timu ya Taifa ya Ubelgiji kwaajili ya Mtanange wa Kombe la Dunia.
++++++++++++++++++++++++++++

No comments