THE GUNNING MACHINE ~ WIMBO MTAMU WA ARSENAL KWA SASA NI WEMBLEY!! WEMBLEY!!! WEMBLEY!!!


Zikiwa zimesalia mechi 5 tu kwa Arsenal kumaliza msimu huu katika ligi kuu Nchini England, hali ya kupatikana kwa ubingwa imekua ndoto baada ya matokeo mabaya ya mwezi Machi. Na pengine mwezi Machi utakua umechukiza wengi baada ya kuleta matokeo mabaya yaliyoipeleka Arsenal kutoka namba moja mpaka sasa kugombania nafasi ya kuingia katika timu nne bora.

THE GUNNING MACHINE Inaamini wimbo mzuri kwa mashabiki wa Arsenal kwa kipindi hiki ni Wembley!! Wembley!! Wembley!! Yes hapa nazungumzia nafasi ya Arsenal kushinda kombe la FA katika uwanja wa Wembley baada ya kusubiri tangu mwaka 2005 bila kombe lolote na pengine kama litapatikana kombe hili basi yaweza kua njia ya kupatikana makombe mengine mbeleni.

Zikiwa zimebaki mechi 5 kukamilisha msimu huu hakuna matumaini ya kubeba Ubingwa wa Ligi nchini England lakini kuna uwezekano mkubwa wa kubeba kombe la FA
Arsenal inakutana na Wigan katika hatua ya Nusu Fainali Jumamosi ya leo mchezo utakaoanza saa 1 Usiku katika dimba la Wembley.

Ni dhahiri hiki ni kikwazo kingine kwa Arsenal katika ndoto zake za kuwa bingwa mpya wa Kombe lenye historia kubwa katika Soka Yani Kombe la FA kwani Wigan ndo timu iliyoitoa Manchester City katika uwanja wa Etihad huku wengi wakiamini kama Man City walikua na nafasi ya kuchukua kombe hili.

Arsenal inaingia katika mchezo wa leo ikiandamwa na majeruhi kadhaa wakiwemo Mesuit Ozil,Wilshere, Koscienly, Theo Walcott huku pia wachezaji kama  Alex Oxlade-Chamberlain,Tomas Rosicky na Kieran Gibbs wakiwa na hatihati ya kucheza mechi hiyo kutokana na majeruhi.


Kumekua na hisia tofauti miongoni mwa mashabiki na wachezaji wa zamani wa Arsenal wengi wakiamini bora kukosa nafasi ya kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao lakini kuibuka na kombe hili na mmoja wa Magwiji hao ni Ray Parlour mchezaji wa Zamani wa Arsenal ambaye ameshinda ubingwa wa ligi mara 3 na ule wa kombe hili mara 4 akiwa na Arsenal.

Lakini Kocha Arsene Wenger alipoulizwa kama angechagua kipi kati ya TOP 4 na Kombe la FA yeye alijibu "Kama Kocha hupaswi kuchagua bali unapaswa kujenga kikosi imara cha kufanya vizuri kwa mechi zilizobaki" japokua bado wengi pia tunaamini ili Wenger awe na amani msimu ujao ni bora akachukua kombe hili.

FACTS
  • Arsenal na Wigan hazijawahi kukutana katika michuano hiyo ya kombe la FA ila kwa mara zote ambazo Arsenal imewahi kukutana na Wigan Arsenal imeshinda mara 15 kati ya 20 huku Wigan wakishinda mara 3 na sare zilikua 2.
  • Olivier Giroud amefunga Goli 5 katika mechi 5 zilizopita katika kombe la FA yakiwemo magoli matatu katika mechi 3 ambazo aliingia kipindi cha pili.
  • Arsenal imepoteza mechi zote Mbili walizocheza katika uwanja wa Wembley tangu uwanja huo ufunguliwe upya mara ya kwanza ikiwa mwaka 2009 katika nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Chelsea ikikubali kipigo cha 2-1 na mwaka 2011 walipopoteza katika fainali ya kombe la Ligi wakati huo likiitwa Carling Cup dhidi ya Birmigham City.
  • Arsenal itabidi iwe makini na Wigan kwani timu hii imeshinda mechi zote mbili walizocheza katika dimba la Wembley ikiwemo fainali ya mwaka jana dhidi ya Man City.
Kilichobaki ni kusubiri kuona jinsi ambavyo kikosi cha Arsene Wenger kitavuka kikwazo hiki na kutinga fainali na kisha kuchukua kombe ili kusahau machungu ya kusubiri kwa miaka 9 bila kombe lolote kitu ambacho ni aibu kwa klabu kubwa kama Arsenal.
Ikumbukwe hili ndo kombe la mwisho kwa Arsenal kushinda na hili laweza kua kombe la kwanza Arsenal kushinda baada ya ukame wa miaka 9. So wimbo uendelee mpaka kieleweke.

WEMBLEY!!!!! WEMBLEY!!!!! WEMBLEY!!!! WEMBLEY!!!!

.....Na Edo Daniel Chibo

No comments

Powered by Blogger.