ARSENAL HAOOOOOOOOOO FAINALI YA FA. FABIANSKI SHUJAA
Baada ya Miaka 9 Shujaa anajitokeza katika dimba la Wembley huyu si mwingine bali ni kipa raia wa Polandi anayekipiga Arsenal Lucas Fabianski baada ya kuivusha timu hiyo kutinga Fainali ya Kombe la FA alipodaka penati mbili kati ya 4 na kuwapa mashabiki wa Arsenal faraja ya Kufika fainali ya kombe hili huku wakitegemea pengine watalichukua na kufuta wa miaka 9 bila kombe lolote.
Arsenal imeweza kuwatoa Wigan ambao ni mabingwa Watetezi katika hatua hii ya Nusu fainali kwa penati 4-2 baada ya mchezo huo kumalizika dakika 120 huku matokeo yakiwa 1-1.
Wigan ndiyo waliotangulia kuliona lango la Arsenal kwa goli safi kabisa la Penati lililofungwa na Jordi Gomez baada ya Per Metesacker kumwangusha mshambuliaji wa Wigan Mac Manaman ndani ya eneo la hatari ndipo mwamuzi akaamua iwekwe penati.
Goli la Kusawazisha la Arsenal lilipatikana dakika ya 83 kwa mpira wa kichwa uliowekwa kimiani na Per Metersacker.
Penati za Arsenal zilifungwa na Mikel Arteta, Kim Kallstrom, Olivier Giroud na Santiago Carzola huku Wigan wakifunga penati 2 wapigaji wakiwa ni Jean Beausejour na James McArthur huku Jack Collison na Gary Caldwell wakikosa yani Fabianski akizidaka kabisa.
Arsenal imetinga fainali sasa na itamsubiri mshindi wa mechi ya kesho kati ya Hull City na Sheffied United ili kucheza fainali mwezi Mei.

No comments