SAFARI YA MOROCCO MWAKANI, TANZANIA KUMENYANA NA ZIMBABWE
Ndoto ya Rais mpya wa TFF kutaka kuipeleka Tanzania katika fainali zijazo za kombe la Mataifa ya Afrika nchini Moroko mwakani zitaanza kwa kuikabili Zimbabwe katika mechi za awali ambazo zitachezwa nyumbani na ugenini mechi ya awali ikifanyika hapa Tanzania wikiendi ya Tarehe 16-18 Mei kisha marudiano kupigwa baada ya wiki mbili huko Zimbabwe.
Kama Tanzania itavuka kizingiti hiki basi itakutana na mshindi kati ya Msumbiji na Sudani ya Kusini katika mechi nyingine mbili za nyumbani na ugenini zitakazopigwa wikiendi ya Tarehe 18-20 mwezi Julai na marudio yakiwa baada ya wiki mbili huku mechi hizo nazo kama Tanzania itavuka basi zitaanzia nyumbani.
Tanzania ikivuka na hapo basi itaingia katika hatua ya Makundi 7 ambapo washindi wa kwanza na wapili watapata nafasi ya kucheza katika fainali hizo nchini Moroko
Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF lilikutana katika makao makuu yake pale Caira Jumapili kupanga hatua ya Makundi na ratiba nzima ya michuano hiyo ambapo makundi 7 yamepangwa huku kila kundi likitarajiwa kutoa wawakilishi wawili halafu kutakua na timu bora iliyoshindwa kuvuka lakini ina matokeo mazuri (Best Loser) ambayo itaungana na timu hizo 14 pamoja na mwenyeji Moroko kukamilisha idadiya timu 16.
KUNDI LA TANZANIA
GROUP F
Zambia
Niger
Cap Verde
Mshindi wa Tanzania vs Zimbabwe au Msumbiji vs Sudan Kusini.
Mechi za Hatua hii ya Makundi zitaanza kupigwa Septemba 5-6 Mwaka huu
NOTE: Tanzania inaanzia hatua hii kwakua kiwango chetu cha soka bado kiko chini katika Viwango vya soka vinavyotolewa na FIFA.

No comments