LIGI KUU ENGLAND ~ ARSENAL YAJIIMARISHA TOP 4
Goli pekee la kipindi cha kwanza la mshambuliaji Olivier Giroud liliweza kuiweka Arsenal katika nafasi nzuri zaidi katika timu 4 za juu wakati huu Ligi ikiwa inaishia.
Arsenal imeweza kufikisha pointi 76 pointi mbili nyuma ya Chelsea walio katika nafasi ya 3 kwa pointi 78.
Kuna nafasi kubwa kwa Arsenal kupanda mpaka nafasi ya 3 iwapo Chelsea watapoteza michezo yao miwili ya mwisho ukianzia na huu wa leo dhidi ya Timu inayojikwamua isishuke daraja Norwich.
Kama inavyojulikana timu 4 za juu hucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini iliyo katika nafasi ya 4 huanza na mechi za mtoano wakati zile 3 za juu huanza katika makundi moja kwa moja.
~ By Edo Daniel Chibo (WS)
+++++++++++++++++++++

No comments