LIGI YA MABINGWA ULAYA ~ MAN UNITED NA BARCELONA WATUPWA NJE
Usiku mbaya kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England Man United na Wale Mabingwa watetezi wa Spain Barcelona baada ya kutolewa katika hatua ya Robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Man United Ikiwa ugenini nchini Ujerumani Imekubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa Mabingwa Watetezi Bayern Munich katika mchezo ambao Man United walihitaji kufunga goli na kuzuia kutofungwa goli lolote ili wasonge mbele.
Ikishiriki kwa mara ya 18 mfululizo Man United ilifanikiwa kupata goli la kuongoza kupitia kwa Patrice Evra dakika ya 57 kabla ya mario Mandzukic hajasawazisha dakika moja baadae. Thomas Muller aliongeza goli la pili dakika ya 68 kabla ya Robben hajafunga goli la 3 dakika ya 76 na kuifanya Bayern kutinga Nusu fainali kwa ushindi wa Jumla wa goli 4-2.
Katika Mechi nyingine Barcelona wameduwazwa na kasi ya Atletico Madrid baada ya kupigwa 1-0 na Atletico Madrid hivyo kutolewa kwa kipigo cha jumla cha 2-1 baada ya mechi ya kwanza Kumalizika kwa 1-1 katika uwanja wa Barcelona.
Kwa misimu kadhaa iliyopita Imezoeleka kuwa timu inayomtoa Barcelona katika michuano hiyo huwa Bingwa hapa swali ni je Unadhani Atletico Madrid wana kikosi kizuri cha kuchukua ubingwa msimu huu?
Kwa matokeo ya leo Timu nne zimefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali ya michuano hiyo ambazo ni CHELSEA,REAL MADRID,BAYERN MUNICH na ATLETICO MADRID na droo ya Nusu fainali ya michuano hiyo itafanyika siku ya Ijumaa Tarehe 11 April 2014.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments