EPL ~ SPURS YAUA 5-1 NA KUIRUDISHA MAN UNITED NAFASI YA 7 HUKU ADEBAYOR AKIIBUKA SHUJAA
Akirudi rasmi toka majeruhi, Mshambuliaji raia wa Togo anayekipiga Totenham Hottspurs Emmanuel Adebayor ameibuka shujaa katika mchezo wa Ligi kuu nchini England baada ya kupiga goli 2 katika ushindi wa bao 5-1 walioupata Totenham Hottspurs dhidi ya Sunderland.
Iliwachukua Sunderland dakika 17 tu kuandika bao katika Uwanja wa White Hart Lane kupitia kwa Lee Cattermole goli ambalo liliwazindua toka usingizini Tottenham na kujibu mashabulizi na kufanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya 28 likiwekwa kimiani na Emmanuel Adebayor na mpaka Mapumziko ilikua 1-1.
Kipindi cha pili Mshambuliaji kinda wa Spurs Harry Kane dakika ya 59 aliwainua mashabiki badaa ya kufunga goli la pili, Baadaye dakika ya 78 Christian Eriksen alifunga bao la 3 kabla ya Adebayor hajafunga la 4 huku Gylfi Sigurdsson akifunga bao la 5 dakika za lala salama.
Kwa Matokeo hayo Spurs inairudisha Man United katika nafasi ya 7 kwenye msimamo kwani Spurs imefikisha pointi 59 mbili zaidi ya zile za Unitedna hii inazidi kuongeza presha katika kuwania nafasi ya kukamata nafasi ya 4 kwani Everton,Arsenal na United wanapigania kuipata.
Kwa Upande wa Sunderland haya matokeo yanawaweka pabaya kwani wamebaki na pointi zao 25 katika nafasi ya mwisho huku ikiwa na mechi mbili mkononi kama viporo.
....Na Edo Daniel Chibo
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments