LIVERPOOL YAIVUA RASMI UBINGWA MAN UNITED

>  UBINGWA SASA NI KWA LIVERPOOL, MAN CITY AU CHELSEA


Ushindi wa bao 2-1 walioupata Liverpool hidi ya West Ham United katika pambano la Ligi kuu Nchini England limeivua Rasmi taji hilo waliokua mabingwa Watetezi Manchester United ambao walilitwaa mwaka jana.

Tangu ligi kuu ya England kubadilishwa mfumo wake mwaka 1992/1993 Liverpool haijawahi kutwaa taji hilo  na mwaka huu wameonekana kulikaribia baada ya kufanya vizuri katika mechi zake msimu huu hasa mwaka 2014 baada ya kushinda mechi zote tangu mwaka huu Uanze.

Kwa ushindi huo dhidi ya West Ham ambao Liverpool walishinda kwa magoli ya Penati mbili za Steven Gerard Liverpool imerudi kileleni mwa ligi Kuu baada ya kujikusanyia pointi 74 pointi ambazo hata kama Manchester United watashinda michezo yao yote mitano iliyobaki haiwezi kuzifikia.

Hivi sasa Baada ya mechi 33 Man United inakamata nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 57 na hii ni kusema Rasmi kama Liverpool wameivua United ubingwa msimu huu na vita iliyobaki hivi sasa ni kugombania nani atakua bingwa Mpya kati ya Liverpool wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 74, Chelsea wanaokamata nafasi ya pili hivi sasa kwa kua na pointi 72, Manchester City wao wako katika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 70 lakini Man City wao wakiwa wameshacheza mechi 31 tu.

Arsenal wanaokamata nafasi ya 4 wakiwa na pointi 64, Everton walio na pointi 63, Man United walio na Pointi 57 pamoja na Totenham walio na pointi 56 wako katika nafasi nzuri ya kugombea nafasi moja ya kuuungana na timu 3 za Juu katika kutafuta nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Mwakani.

Je Nani ataibuka Bingwa mpya wa Ligi hii inayopendwa zaidi Duniani?

.....
Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo

No comments

Powered by Blogger.