EPL ~ MASHABIKI ARSENAL WALIA NA KOCHA ARSENAL WENGER WENGI WATAKA AONDOKE
Katika hali inayoonyesha kuchukizwa na mwenendo mbaya wa timu yao, Mashabiki wengi wa Arsenal wamechoka na kocha wao Arsene Wenger na wengi kupitia mitandao mbali mbali wakimlaumu na kumtaka aondoke na shinikizo limeongezeka zaidi mara baada ya kipigo cha Ugenini cha bao 3-0 toka kwa Everton na kufanya ndoto yao hata ya kucheza katika ligi ya mabingwa Ulaya kwani Everton sasa wanawakimbiza katika kuwania nafasi nne bora za juu.
Everton inakamata nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 63 lakini ikicheza michezo 32 wakati Arsenal wanakamata nafasi ya 4 wakiwa na pointi 64 huku wakiwa wamecheza mechi 33 Hapo ndo linapokuja Tatizo kwa mashabiki wa Arsenal kwani miezi michache iliyopita timu ilikua ikiongoza ligi kwa tofauti ya pointi nyingi tu lakini hivi sasa wanagombania nafasi ya 4.
Magoli ya Everton jana yaliwekwa kimiani na Steven Naismith dakika ya 14 kabla ya Romelu Lukaku hajafunga la pili dakika ya 34. Mikel Arteta alikamilisha kipigo hicho baada ya kujifunga goli dakika ya 61 ambalo liliwazamisha kabisa Arsenal na kuwafanya kufikisha mechi ya 7 ikifungwa msimu huu, Ikiwa imeshashinda mechi 19 na kutoa sare mechi 7 huku ikiwa imeshafunga magoli 56 na kuruhusu kufungwa magoli 40.
Nafasi ya 4 sasa imeingia katika ushindani mpya kwani Man United walio na pointi 57 na Totenham Hottspurs walio na pointi 56 wako katika mbio za kuwania nafasi hiyo adimu ambayo ni tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hivyo kufanya vita ya kuwania TOP 4 safari hii kuwa kwa timu 4 ambazo zote ziko vizuri.
Swali ni kwamba Unadhani wanaosema Wenger aondoke wako sahihi?
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments