LIGI KUU YA ENGLAND ~ TIMU ZA MANCHESTER ZAFANYA MAUAJI
Magoli 8 yamefungwa na Klabu kutoka Jiji la Manchester leo katika mwendelezo wa hatua ya mechi za lala salama kabla ya kumaliza msimu huu wa Ligi wakati Manchester City wakiwania nafasi ya kuwa mabingwa Wapya huku wenzao Manchester United wakitafuta japo nafasi ya 4 katika msimamo, wakiibuka wote na ushindi wa jumla wa mabao 8 kila mmoja akigawana sawa yani goli 4
Manchester City wakiwa nyumbani wameweza kuitungua Southampton bao 4-1 na kupanda mpaka nafasi ya Pili ya msimamo wa ligi ikiwa na pointi 70 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi. City wanakamata nafasi ya pili pointi moja pungufu ya Liverpool wanaoongoza katika ligi hiyo.
Man City wameweza kupata magoli yao kupitia kwa Yaya Toure dakika ya 4, Samir Nasri Dakika ya 45, kabla ya Dzeko hajamaliza kwa kufunga goli moja kabla ya mapumziko. Steven Jovetic akiipatia City bao la 4 huku lile la Southampton likifungwa na Lambert kwa penati.
Kwa upande mwingine wa Jiji la Manchester mabingwa watetezi Man United walisafiri mpaka St. James park kuikabili NewcastleUnited na hatimaye kuibuka na ushindi wa bao 4-0 huku ikiwaacha wachezaji wake 8 wa kikosi cha kwanza ili kujiweka sawa na mechi dhidi ya Bayern Munich katika hatua ya Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki.
Magoli ya United yalifungwa na Juan Mata magoli mawili, Chicharito naye akafunga moja huku Adnan Januzaj akimalizia kazi kwa kufunga bao la 4 baada ya kugongeana vyema na Mata.
Kwa matokeo hayo Man United imepanda kwa nafasi moja katika msimamo wa ligi ambapo sasa inakamata nafasi ya 6 ikiwa na pointi 57.
Matokeo mengine ya Ligi kuu England ni kama Ifuatavyo:-
- Cardiff City 0-3 Crystal Palace
- Norwich 0-1 West Brom
- Hull City 1-0 Swansea City
- Aston Villa 1-2 Fulham

No comments