LALIGA ~ ATLETICO MADRID YAKOMAA KILELENI HUKU BARCELONA WAKIPIGA 3 NYUMBANI



Katika hali inayoelekea kutaka kuondoa utawala wa Real Madrid na Barcelona katika Soka la Hispania, Klabu ya Atletico Madrid kwa mara nyingine imezidi kukomaa katika nafasi ya kwanza baada ya leo kuinyuka Villareal kwa bao 1-0 goli lililofungwa na Raul Garcia dakika ya 14 ya Mchezo.

Atletico Madrid inayofundishwa na Diego Simeone imejikuta ikiwaongoza wababe wa Soka la Spain kwa kukamata nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 79 pointi moja Juu ya mabingwa watetezi Barcelona ambao nao wameweza kushinda kwa bao 3-1 dhidi ya Real Betis leo hii.

Barcelona ambao watakutana na Atletico Madrid katika mechi ya raundi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mechi ya Pili siku ya Jumatano ilifunga magoli yake kupitia kwa Lionel Messi aliyefunga magoli mawili ya penati huku Betis wakijifunga goli moja.

Real Madrid wao Usiku huu wako uwanjani kuwakabili Real Sociedad katika mechi nyingine kubwa ya La Liga.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.