RASMI: LIGI KUU YA VODACOM YARUDI SHINYANGA NA MTWARA HUKU JULIO AKICHEMKA KUIPANDISHA MWADUI FC
Miaka 13 imepita tangu mji wa Shinyanga kushuhudia mitanange ya ligi kuu Tanzania Bara na sasa faraja imekuaja baada ya Stendi United kupanda rasmi daraja na sasa itacheza ligi kuu Tanzania bara.
Stendi imefanikiwa kupanda daraja baada ya kupata pointi za "mezani" kufatia Rufaa yake dhidi ya Kanembwa JKT kukubalika na hivyo basi kupata pointi 3 na magoli mawili.
Stendi United ilikua ikigombea nafasi ya kupanda daraja katika kundi C ikikamata nafasi ya pili kabla ya mechi za leo ikiwa na pointi 26 huku Mwadui kabla ya mechi za leo wakiongoza ligi hiyo kwa pointi 28 hivyo basi ushindi pekee wa Mwadui ungewapeleka Ligi kuu.
Mwadui Inayonolewa na Jamuhuri Kiwelu "Julio" ikiwa mjini Dodoma leo iliweza kuinyuka Polisi ya mjini humo kwa bao 2-1 ushindi huo ambao umekifanya kikosi cha Mwadui kufikisha point 31 ambazo zisingeweza kufikiwa na timu yoyote katika kundi hilo.
Kwa upande wao Stendi United walikua Kambarage Shinyanga wakiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Toto Africa matokeo ambayo yaliifanya Stendi United kufikisha pointi 29 na mara baada ya kusikilizwa Rufaa yao na kupewa pointi 3, Stendi waliweza kufikisha pointi 32 na kuongoza kundi hilo ambapo sasa wanaungana na Ndanda FC ya Mtwara na Polisi Morogoro kuingia katika ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments