THE GUNNING MACHINE ~ HESHIMA YA MECHI YA 1000 KWA WENGER NI KUIFUNGA CHELSEA LEO.

 
Arsenal leo itaingia kucheza na Chelsea katika mechi ya Ligi kuu nchini England kwa namna ya kipekee kabisa kwani mzee wetu Arsenal Wenger atakua akifikisha mechi yake ya 1000 tangu alipoanza kuifundisha Arsenal.

Team ya nzima ya waandaaji wa makala hii ya THE GUNNING MACHINE wanapenda kumpongeza mzee WENGER kwani Hii ni heshima kubwa kwa kocha kuweza kudumu kwa kipindi hiki chote akiwa na timu moja tena kwa mafanikio makubwa. 

Mechi 500 za kwanza kwa Mzee Wenger ndizo hasa zilizompatia mafaniko kwani ndani ya mechi hizo 500 Wenger alifanikiwa kuchukua vikombe 11 yani Ubingwa wa ligi kuu England EPL mara 3, Kombe la FA mara 4 na Ngao ya Hisani mara 4.

Japokua kwa mechi 499 baada ya hizo za awali kutopata kombe lolote bado Wenger anaheshimika kwa kuisaidia Arsenal kumaliza Top 4 kila msimu hii ni tofauti na vilabu vingine ambavyo vimeshindwa kufanya hivyo.

Ushindi katika Mchezo wa leo dhidi ya Chelsea ni zawadi pekee kwa kocha Arsenal Wenger katika siku hii maalumu kwake lakini THE GUNNING MACHINE Inaamini kuwa kupata Ushindi katika dimba la Stamford Bridge si kazi rahisi kwani Historia ina mengi ya kutuambia zinapokutana timu hizi zote zikitoka jiji la London
  • Arsenal imeshatembelea Darajani mara 76 na katika mara hizo Arsenal Imeshinda 25 ikatoa sare mara 25 na kupoteza mara 26 huku Ikifunga goli 100 wakati Chelsea wao wameweka kambani magoli 95.
  • Arsenal haijawahi kuifunga Chelsea katika mechi 4 zilizopita baina ya timu hizo huku Chelsea ikishinda 2 na kutoa sare 2.
  • Huu ni mchezo wa 11 wa kocha Arsene Wenger kukutana na kocha wa Chelsea Jose Mourinho na katika mara 10 zilizopita Mourinho akishinda mara 5 wakati Wenger hajawahi kushinda na sare zimepatikana mara 5
  • Haitakua kazi rahisi kuifunga Chelsea katika uwanja wa nyumbani kwani Mara ya mwisho Chelsea walipofungwa katika ligi wakiwa katika huo uwanja wao wa nyumbani ilikua Januari mwaka 2013 dhidi ya QPR na kuanzia wakati huo Chelsea imecheza mechi 25 nyumbani bila kufungwa.
  • Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikua Disemba mwaka jana katika Dimba la Emirates na mchezo jhuo uliisha kwa sare ya 0-0.
  • Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamefunga kila mechi isipokua mechi moja tu kati ya mechi 15 msimu huu na timu iliyofanikiwa kutofungwa hapo ilikua West Ham Januari mwaka huu sasa kwa washambuliaji wetu pale wataweza kweli kufunga huku wakina Per na Koscienly wasiruhusu kufungwa?
Arsenal inaingia katika mchezo wa leo ikikabiliwa na majeruhi kadhaa wakiwemo Aaron Ramsey, Jack Wilshere, Theo Walcott na Abou Diaby. Huu ni mchezo sio tu utakaoweza kumpa furaha Wenger kwa kufikisha mechi 1000 lakini pia huu ni mchezo muhimu katika kuwania ubingwa msimu huu kwani wiki Ijayo kazi itahamia kwa Man City. Kufungwa katika mechi hii itamaanisha nafasi itakua finyu ya kunyakua ubingwa.

Kwa leo tunaishia hapa tukutane Jumamosi Ijayo katika THE GUNNING MACHINE nyingine.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.