LIGI YA MABINGWA ULAYA ~ VAN PERSE AMPA MOYES MKATABA WA MAISHA OLD TRAFFORD.


RVP akifunga goli la 3

Katika hali isiyotogemewa na wengi, Kocha wa Manchester United David Moyes amekiongoza kikosi cha timu hiyo kutinga hatua ya Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kupokea lawama nyingi kwa matokeo mabaya yanayoendelea kuikumba timu hiyo.

Shujaa wa United Robin Van Perse pengine atashukuliwa sana na Moyes kwani magoli matatu yake yameweza sio tu kuivusha Man United kuingia Robo Fainali lakini pia kupunguza presha kwa kocha David Moyes ambaye ilisemekana amepewa mechi 3 Kuanzia ile ya jana na kipoteza basi pengine angeonyeshwa mlango wa kutokea japo haikuthibitishwa na uongozi wa Man United.

Man United iliingia katika mchezo wa jana huku ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa bao 2-0 katika mchezo wa awali hivyo basi ilipaswa kushinda 3-0 ili  kuvuka na ndicho kilichofanyika.

Robin Van Perse alianza kufunga bao la kwanza kwa penati dakika ya 22 kabla ya kufunga lingine dakika ya 45 na mpaka mapumziko United walikua mbele kwa bao 2-0.
Kipindi cha pili Robin Van Perse alifunga bao la tatu ambalo liliwapa nafasi ya kutinga Robo Fainali kwa mpira wa adhabu ndogo nje kidogo
ya boksi la 18 baada ya Welbeck kufanyiwa adhabu.


Kwa matokeo hayo Man United inaungana na Chelsea kutoka katika Ligi kuu ya England kuingia katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kukamilisha timu 8 za hatua ya Robo fainali katika droo itakayopangwa kesho.

Katika mechi nyingine ya hatua hiyo Zenit ya Russia ilikua ugenini na kuifunga Dortmund 2-1 ila ushindi huo haujaisaidia kwani imeweza kutolewa kwa matokeo ya jumla ya 5-4 baada ya kufungwa 4-2 mechi ya awali kule Russia.

Timu zote ambazo zimeingia katika hatua hii ni Chelsea, Man United,Barcelona, Atletico Madrid, Real Madrid, Bayern Munich,Borussia Dortmund na PSG.

++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.