MIWANI PANA YA EDO ~ SABABU 5 ZA KUISHANGILIA YANGA LEO
![]() |
| kikosi cha Yanga |
Unapomwambia mshabiki wa Simba aishangilie Yanga ni kujitafutia Ugomvi na mabishano yasiyo na tija vivyo hivyo shabiki wa Yanga kuishangilia Simba. Huu ni utaratibu uliojengeka kwa miaka mingi sana nadhani sio Tanzania tu bali duniani kote japokua Tanzania Imezidi kwani mashabiki wa timu pinzani husimama na kuishangilia timu ngeni wakati nchi nyingine mashabiki huamua kukaa kimya na kutoshangilia kabisa timu yoyote nadhani hii pia ingejitokeza leo ingewasaidia sana wachezaji kuongeza morali ya ushindi.
MIWANI PANA YA EDO leo imejikita kuangazia sababu 5 zinazoweza kukushawishi kuishangilia Yanga leo:-
- UMUHIMU WA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA
Katika bara la Afrika hii ndiyo michuano mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu na ushindi pekee kwa Yanga hasa kuwafunga mabingwa watetezi wa kombe hilo sio tu itakua habari kubwa hapa Tanzania bali Duniani kote na mustakabali wa soka la Bongo.
Hapa naongelea Yanga ikicheza na mabingwa wa Afrika Al Ahly haichezi na JKT Oljoro au Mgambo Shooting hivyo basi ni wajibu wako kama Mpenda Soka kuipa sapoti hata kwa kukaa kimya tu ukiwa uwanjani na sio kuwashangilia Waarabu.
Nani anaifahamu Tanzania katika Soka? Ni ngumu kwakua hatua balozi katika soka letu nje ya nchi sasa hii ndiyo nafasi tosha ya kututangaza kama Huku Tanzania na sisi tupo na hii pia ni nafasi ya wachezaji wenye ndoto za kucheza Nchi zilizoendelea watakapoonekana katika mechuano hii.
- NAFASI YA KUPATA TIMU TATU KUIWAKILISHA NCHI AFRIKA
Hivyo basi kama Yanga itafanya vizuri katika michuano ya mwaka huu na kufika japo Nusu fainali hii Itaongeza ushiriki kwa timu za Tanzania katika michuano inayoandaliwa na shirikisho la Soka barani Afrika CAF na kuongeza wigo wa ligi yetu kwa timu itakayokamata nafasi ya 3 nayo kushiriki mwakani na kama Yanga ikitolewa mapema basi ni dhahiri tutaendelea kuwa pale pale huku tukijifurahisha na ligi yetu. Hiyo ni sababu nyingine tosha ya kuishangilia Yanga leo.
- UWEZO WA YANGA NDANI YA UWANJA
Yanga imetulia katika uongozi na kipesa kwasasa huku wakifanya usajili wa makini utakaoweza kuisaidia katika michuano hiyo na hapa nawazungumzia wachezaji kama Emmanuel Okwi,Mrisho Ngasa, Hamis Kiiza,Juma Kaseja,Didie Kavumbagu, Huruna Niyonzima n.k ambao uwepo wao katika kikosi cha Yanga utaisaidia sana kwani ni wachezaji wenye 'Experience" na soka la Afrika hivyo unapoipa sapoti huna che kupoteza kwani ni nadra kwa "kaliba" ya wachezaji hao kukuangusha.
Yanga ni timu pekee toka Tanzania iliyobaki katika mashindano hayo huku maandalizi yake yakiwa ni ya kuridhisha.
- VITA KUBWA TULIYONAYO NA TIMU ZA KIARABU
Utawapendaje Waarabu bana katika mpira huku ukiwa na wachezaji pendwa nchini mfano ni wachezaji kama Emmanuel Okwi, Juma Kaseja na Mrisho Ngasa hao wamekipiga msimbazi na kila mmoja aliwafurahia sasa nini kinabadilika kwao uanze kuwachukia na kuwazomea leo?
- USHINDI WA MAGOLI 12 KATIKA MECHI MBILI
Yanga imeingia hatua hii ya pili ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuitoa timu toka Comoro kwa kuwafunga magoli 12 nadhani huu ni ushindi mkubwa kabisa barani Afrika katika hatua hiyo hii inaonyesha kabisa Yanga wana uwezo mkubwa wa kufunga na kama Utaenda Uwanja wa Taifa ni dhahiri unaweza kumwona Ngasa akicheka na Nyavu tena baada ya kupiga 6 katika magoli hayo 12 hatua iliyopita.
Kufunga magoli mengi imekua ugonjwa kwa wachezaji wa Tanzania sasa inatia hamasa sana kuona Mtanzania mwenzetu akiwa anaongoza list ya Wafungaji bora wa ligi ya Mabingwa barani Afrika.
MIWANI PANA YA EDO Inaishia hapa kwa leo tukutane tena siku nyingine
..... Kwa maoni na Ushauri usisite kuniandikia
Email: mfalme.edo@gmail.com
Facebook: Edo Daniel Chibo
Twitter: Edo Daniel1
Page: Wapenda Soka - Kandanda
Whatsapp: +255 715 12 72 72


No comments