MIWANI PANA YA EDO ~ MZIMU WA KOMBE LA FA KUWAOKOA ARSENAL NA UKAME WA MAKOMBE?
Mwaka 2005 Wapenda Soka wengi ambao leo wako katika makundi ya Soka katika mitandao mbalimbali ya jamii hasa facebook likiwemo kundi mama la Blog hii (Wapenda Soka (Kandanda)) walikua bado wako vyuoni na mashule mbalimbali tena wengine walikua bado wako Shule za msingi hapa najua mshkaji wangu Allen Kaijage na Adin Lwekika hawawezi kubisha mana wanahusika sana.
Wengi tulikua hatuijui Facebook ambayo ilikua ni mwaka mmoja tu ilipoanzishwa na wengi wetu ndo tulikua tumeanza kumiliki simu za mkononi ambazo sikumbuki kama zilikua na Internet wakati huo.
Mwaka 2005 ni mwaka ambao Arsenal kwa mara ya mwisho walishinda kombe tena likiwa kombe la FA walipoifunga Manchester United katika uwanja wa Millenium uliopo Cardiff Wales kwa mara ya Tano mfululizo kufanyika katika uwanja huo baada ya uwanja wa Wembley kuwa katika matengenezo. Kilikua kikosi bora kabisa katika historia ya Ligi kuu Nchini England ambacho kilimaliza msimu uliopita kabla ya msimu wa 2004/2005 kwa kutofungwa mchezo wowote katika Ligi Kuu nchini England hadi kua mabingwa.
May 21,2005 Dakika 90 za Fainali ya kombe la FA kati ya Arsenal na Manchester United zilimalizika kwa sare tasa yani 0-0 na hata zilipoongezwa zile 30 bado hakuna timu iliyoweza kufunga goli ikiwa ni Fainali ya kwanza kuisha kwa sare ya bila kufungana mara ya mwisho Fainali ya kombe hilo ambayo iliisha bila kufungana ilikua mwaka 1912 hivyo basi mechi iliamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Arsenal walishinda penati 5-4 ikiwa ni timu ya kwanza katika historia ya michuano hiyo kushinda kwa penati.Hilo ndo lilikua kombe la mwisho kunyakuliwa na Arsenal chini ya Arsene Wenger na Tangu wachukue kombe hilo imekua kama "gundu" kwao kwani tangu wakati huo hawajafanikiwa kushinda kombe lolote japokua wameweza kufika Fainali mbili moja ikiwa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakifungwa 2-1 dhidi ya Barcelona mwaka 2006 baadaye wakapoteza tena kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Birmigham City katika kombe la Ligi maarufu wakati huo kama Carling Cup. mwaka 2011.
Mwaka Huu Arsenal wameanza msimu vizuri kwa kuongoza kwa muda mrefu katika msimamo wa ligi kuu ikiwapa matumaini mashabiki wao kama huu ni mwaka wao lakini kadri siku zinavyosogea ndipo mambo yanabadilika kwa Timu hiyo ikiwa na majeruhi wengi hivyo kuwa na matumaini finyu kuhusu kunyakua ubingwa katika Ligi kuu. Kombe pekee ambalo linaonekana laweza kua rahisi kwao baada ya kuvuka vikwazo vyote ni kombe la FA kwani watakutana na Wigan katika hatua ya Nusu fainali itakayopigwa katika uwanja wa Wembley wakiwatoa Wigan basi watatinga fainali kucheza na msindi kati ya Hull City na Sheffield United.Kama Arsenal watafanikiwa kunyakua kombe hilo basi itakua wameuzika Rasmi mzimu wa kukaa miaka 9 bila kombe mzimu uliowekwa kwa kuchukua kombe hilo hilo mwaka 2005 na pengine likawa kombe la kuuzika rasmi "mzimu" wa ukame na kufungua ukurasa mpya wa makombe ndani ya Emirate. JE WATAWEZA?
...... Tukutane tena wakati mwingine katika MIWANI PANA YA EDO
Usisite kunicheki:-
Edo Daniel Chibo ( Facebook)
mfalme.edo@gmail.com (Email)
Copyright: @Wapenda Soka (Kandanda) 2014.

No comments