BAADA YA ARSENAL KUUA 4 JANA LEO NI ZAMU YA MAN CITY?


Mauaji ya bao 4-1 waliyoyafanya Arsenal dhidi ya Everton jana yameivusha timu hiyo mpaka nusu fainali ya kombe la chama cha soka nchini England (FA) kombe ambalo ni maarufu  na lenye historia kubwa.

Magoli mawili ya mshambuliaji aliyeingia kipindi cha pili Olivier Giroud, Moja la penati ya Mikel Arteta na moja la kiungo mshambuliaji Mesut Ozil yalitosha kuwapa matumaini vijana wa Arsene Wenger ambao wana ukame wa makombe kwa mwaka wa tisa sasa.

Leo katika mechi zingine tatu za hatua hiyo ya Robo fainali itashuhudia Manchester City ambao wameshachukua kombe moja msimu huu wakiialika Wigan Athletic mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Etihad kuanzia saa 2 na dakika 5 usiku hii ikiwa ni kumbukumbu ya msimu uliopita ya Fainali ya kombe hilo ambapo City walifungwa na kuwapa Wigan ubingwa wa FA Cup.

Hull City wataikaribisha Sunderland katika mchezo utakaoanza saa 12 jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki wakati mchezo wa mapema kabisa leo mida ya saa 10 kamili jioni itazikutanisha Sheffield United na Chalton athletic.

Washindi wa mechi za leo watatinga katika hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.