LIGI YA MABINGWA ULAYA ~ ARSENAL NA AC MILAN WAMEKUBALI YAISHE



Mechi za mzunguko wa pili wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ziliendelea jana usiku katika viwanja viwili tofauti kuwa katika wakati mgumu ambapo Miamba ya Soka Barani humo AC Milan na Arsenal walikubali yaishe na kurudi nyumbani kuendelea na mambo mengine.

Arsenal ya England ikisafiri mpaka Ujerumani ilijitaidi kupata Sare ya bao 1-1 na mabingwa Watetezi Bayern Munich katika pambano lililopigwa katika dimba la Alianz Arena ambapo sasa Arsenal wametolewa kwa matokeo ya jumla ya 3-1 baada ya Bayern kuibuka na ushindi wa 2-0 wiki mbili zilizopita jijini London.

Bayern Munich walitangulia kufunga kwa bao la dakika ya 55 kupitia kwa Bastan Schweinsteiger kabla ya Lucas Podoski kusawazisha dakika mbili baadae matokeo yanayoipeleka Bayern Munich Robo fainali na kuwaacha Arsenal wakirudi nyumbani kutafuta nafasi ya kushiriki tena msimu ujao.

Mechi nyingine ilishuhudiwa AC Milan wakipigwa 4-1 na wenyeji Atletico Madrid katika mchezo uliopigwa katika dimba la Vicente Calderon matokeo yanayoivusha Madrid kwa ushindi wa Jumla wa bao 5-1 baada ya kushinda 1-0 katika mchezo wa awali katika dimba la San Ciro jijini Milan.

Magoli mawili ya mshambuliaji aliye katika kiwango cha juu hivi sasa Diego Costa, Moja la Arda Turan na Raul Garcia yalitosha kuwapeleka nje ya michuano hiyo AC Milan waliopata goli la kufutia machozi kupitia kwa Kaka.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.