LIGI KUU TANZANIA BARA ~ USHINDI PEKEE KWA AZAM FC LEO DHIDI YA YANGA SC UNAWEZA KUWAPA UBINGWA TANZANIA
Ndoto ya Klabu ya Azam FC ya Dar Es Salaam kuchukua ubingwa mikononi mwa Yanga inaingia patamu hii leo ambapo wataivaa Yanga ambao ni mabingwa Watetezi wa Ligi kuu katika mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar.
Zamani watu walikua wakiangalia mechi mehi moja na kuipa thamani kubwa yani Simba vs Yanga lakini hali sasa imebadilika mechi hii inaweza kuwa kama ya wapinzani wa jadi.
Kwa miaka mingi sasa timu pacha za Tanzania yani Yanga na Simba zimekua zikipokezana ubingwa wa Ligi huku timu nyingine zikiachwa kuwasindikiza lakini mwaka huu mambo yamebadilika baada ya Azam FC kukaa kileleni mwa ligi huku ikibaki michezo michache kukamilisha ligi na kama Azam itakomaa mpaka mwisho basi wataweza kushinda ubingwa huo.
Kwa Upande wao Yanga mechi ya leo ni muhimu kwao katika harakati za kutetea ubingwa wao wa ligi baada ya kutolewa katika ligi ya mabingwa Afrika. Kama Yanga ikishinda leo itakua nyuma kwa pointi moja tu dhidi ya Azam wanaoongoza ligi hiyo.
Azam Fc Inaongoza ligi kuu Tanzania bara baada ya kucheza michezo 19 ikishinda michezo 12, Imetoa Sare michezo 7 na ndo timu pekee ambayo haijafungwa mchezo wowote mpaka sasa ikifunga magoli 39 huku ikiruhusu wavu wake kuguswa mara 12 na Ina pointi 43.
Yanga SC ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara wao wamejikusanyia point 39 katika nafasi ya pili wakiwa sawa na Mbeya City. Yanga imecheza mechi 18 ikishinda mechi 11 ikitoa sare mechi 6 na kufungwa mechi moja ambayo walifungwa na hao hao Azam FC. Yanga ndo timu iliyofunga magoli mengi zaidi katika ligi ikifunga magoli 41 huku ikiruhusu kufungwa magoli 12.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika Ligi Yanga walikubali kichapo cha bao 3-2 na kama Azam FC Leo atashinda basi atafikisha jumla ya pointi 46 pointi 7 mbele ya Yanga kitu ambacho kinaweza kuwasaidia kupata ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya kuusotea mwaka jana na mwaka juzi na kuishia nafasi ya 2.
Mchezo huu unaanza saa 10 na utarushwa live na Azam TV.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

team neutral today.
ReplyDelete