JE CHELSEA NDIYO TIMU PEKEE ITAKAYOIWAKILISHA LIGI KUU NCHINI ENGLAND KATIKA ROBO FAINALI?


Ushindi wa bao 2-0 walioupata Chelsea jana Usiku katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora na kuivusha kwa jumla ya goli 3-1 dhidi ya Galatasaray ya Uturuki katika dimba la Darajani umeifanya klabu hiyo kuwa ya kwanza kutinga hatua ya Robo fainali kwa timu kutoka ligi kuu nchini England.

Baada ya Arsenal na Manchester City kutolewa wiki iliyopita timu zilizobaki ni Chelsea na Man United ambayo wengi hawaipi nafasi ya kupita hatua hii baada ya kulambishwa 2-0 na mabingwa wapya wa Ugiriki Olympiacos  katika pambano la awali lililopigwa huko Ugiriki.

Chelsea imeweza kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kupata magoli ya kipindi cha kwanza ya Samuel Eto'o dakika ya 4 na beki wa kati Garry Cahill dakika ya 42 katika mchezo ambao gwiji wa Chelsea Didier Drogba alikaribishwa vyema kwa Mabango na mashabiki wa timu yake hiyo ya Zamani licha ya kuichezea Galatasaray.

Mchezo mwingine wa Ligi hiyo ulishuhudia  Real Madrid wakiifunga 3-1 Schalke 04 Ya Ujerumani katika pambano lililopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu nyumbani kwa Real Madrid.
Mchezaji bora kabisa duniani kwa sasa Cristiano Ronaldo akifunga magoli mawili kati ya hayo matatu na kumfanya kufikisha magoli 42 msimu huu katika michuano yote na kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga zaidi ya magoli 40 kwa misimu minne mfululizo.

Real Madrid wamevuka katika hatua hii kwa ushindi wa jumla wa bao 9-2 na kuifanya kuwa timu pekee msimu huu kufunga mabao mengi katika hatua hii.
Goli lingine la Real Madrid lilifungwa na Morata.

Hatua ya 16 bora ilishuhudiwa timu zote nne toka England zikiingia Yani Man United,Chelsea,Arsenal na Man City lakini mpaka sasa ni timu moja tu iliyoweza kuvuka hatua hii. Spain walikua na timu 3 ambazo zote zishapita yani Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid.
Ujerumani waliingia timu 4 na mpaka sasa ni Bayern Munich pekee iliyopita wakati leo Dortmund watacheza na Zenit.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

3 comments:

Powered by Blogger.