VPL ~ RASMI: AZAM MBABE WA YANGA MSIMU HUU
Mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania kati ya Yanga ambao mabingwa watetezi na makamu Bingwa Azam FC limemalizika kwa sare ya bao 1-1 sare ambayo inaifanya Azam kuwa mbabe wa Yanga msimu huu baada ya kupata pointi 4 kati ya 6 baada ya kushinda 3-2 katika mechi ya mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo wakati Yanga wao wakiambulia pointi 1 tu kati ya pointi 6.
Yanga walitangulia kupata goli kipindi cha kwanza likifungwa na mshambuliaji Raia wa Burundi Didier Kavumbagu huku Azam FC ambao walionekana wako vizuri wakisawazisha kipindi cha pili kupitia kwa chipukizi wa timu hiyo Kelvin Friday.
Yanga itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kushindwa kuutumia mwanya wa Azam FC waliokua pungufu baada ya beki wake Erasto Nyoni kupewa Kadi nyekundu pia Yanga walikosa penati baada ya Hamis Kiiza kupiga penati iliyodakwa na kipa wa Azam, Manula
Kwa matokeo hayo Azam amezidi kujichimbia katika nafasi ya kwanza akiwa na pointi 44 huku Yanga wakibaki katika nafasi ya pili na pointi 40. Mbeya City ni ya Tatu na pointi zao 39 wakati Simba wanakamata nafasi ya 4 na pointi 36.
++++++++++++++++++++++++++++

No comments