MIWANI PANA YA EDO ~ ARSENAL vs MAN UNITED, ILE VITA INAENDELEA


Habari iliyoko mtaani hivi sasa sio zile goli 5 walizofungwa Arsenal Jumamosi wala sio lile goli la Darren Bent dakika za lala buriani ambalo lilizima kabisa na kugeuza Furaha kua huzuni katika uwanja wa Old Trafford Pale Fulham walipotoa sare na mabingwa Watetezi ambao msimu huu umekua mbaya kwao huku Vijana wa mzee Wenger wakipaa katika nafasi za Juu.

Man United inaifata Arsenal huku ikiwa ni ya 7 katika msimamo wa Ligi Ikiwa na pointi 41, Wakati Arsenal Iko katika nafasi ya 2 ikiwa na pointi 55.

KUHUSU HALI ZA WACHEZAJI
 
ARSENAL

Mshambuliaji raia wa Ufaransa Yaya Sanogo yuko sawa na anaweza kucheza katika mechi hiyo baada ya kupona maumivu ya mgongo yaliyomweka nje ya uwanja kwa miezi mitano. Mathieu Flamin hatokuwepo akitumikia adhabu ya kadi nyekundu. Aaron Ramsey, Kim Kallstrom, Thomas Vermaelen, Abou Diaby na Theo Walcott wote hawatakuwepo kutokana na kuwa majeruhi.
Inategemewa kutokua na mabadiliko makubwa katika kikosi kilichofungwa 5-1 na Liverpool

MAN UNITED


  Phili Jones, John Evans,Nani na Fellain Watakua nje ya uwanja kutokana na majeruhi huku Robin Van Perse akianza pamoja na Rooney na Mata kama walivyoonekana katika michezo mitatu iliyopita ya Man United.
HISTORIA INASEMAJE?

 
Historia ipo kwaajili ya watu kukumbuka tulipotoka lakini kamwe haiwezi kuamua matokeo ya leo. Hizi timu zimekua na mashabiki wengi siku hizi na kuongeza msisimko zinapocheza.

  •  Katika Mara 13 zilizopita zilipokutana timu hizo Arsenal wameshinda mara moja tu Goli la Aaron Ramsey mwaka 2011 katika Uwanja wa Emirates huku Man United ikishinda mara 10, Sare zimepatikana mara 2 tu.
  • Kipigo cha 5-1 toka kwa Liverpool kimekua kipigo cha kwanza kwa Arsenal katika ligi msimu huu baada ya kucheza mechi 9 bila kufungwa.
  • Muda kama huu msimu uliopita Man United ilikua ikiongoza Ligi kwa tofauti ya pointi 10 ikiongoza Ligi lakini hivi sasa iko katika nafasi ya 7 ikiwa nyuma kwa pointi 15 chini ya anayeongoza ligi.
  • Arsenal hawajafungwa katika uwanja wao wa Nyumbani tangu waliporuhusu kipigo cha 3-1 katika mechi ya Ufunguzi toka kwa Aston Villa.
  • Robin Van Perse amefunga magoli 7 katika mechi 8 zilizopita na amefunga katika kila mechi zilizocheza timu hizo akifunga mara 2 alipokua Arsenal na amefunga mara 3 akiwa United.
  • Wayne Rooney na Dwight Yorke ndiyo wachezaji walioweka rekodi ya kufunga magoli matatu kila moja kati katika mechi baina ya timu hizo
Kwa Mtazamo wangu nikitumia miwani yangu iliyoongezeka lenzi hii ni mechi ambayo tunaweza kushuhudia timu moja ikifungwa goli nyingi sana ikimbukwe Arsenal hawana forwadi kali kama Man United lakini Man United hawana Beki kali kama Arsenal hasa beki za kati.
Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

4 comments:

  1. Mtizamo binafsi wangu #Jon_Iawr.
    Kwangu ni pambano ninaloliita vita. Ni zaidi ya MTANI JEMBE bongo na ni zaidi ya Riverplate vs Boca Junior.

    Arsenal

    Ninapozungumzia mech hii bwana Edo hatuzungumzii Arsenal yenye ukuta wa Martin Keown wala kiungo mkabaji wa wakati ule Patrick Viera. Hapa ni Arsenal ya kawaida yenye mbinu zile zile kocha yule yule ila kwa watu tofauti. Arsenal wanauchezea mpira ila hawachezi mpira. Hapa ndo inapokuja shughuli anapokutana na Man Utd. Hii mechi kwa Arsenal kama wataingia na hasira ya goli tano toka liverpool basi inawezekana ikawa ni habari nyngne zaidi ya ile iliyowakuta wikiendi. Mchezaji muhmu kwa Arsenal hii leo atakuwa Jack Wilshiere.


    Man Utd

    Historia haina nafasi kwenye soka ila wakati mwngne inakuwa ni changamoto ya kukusogeza kutoka pale ulipoishia. Si mechi nyepesi kwa United ikizingatiwa kuwa perfomance kwa cku za karibuni kwa klabu hii hasa kwa upande wa beki na kiungo ni mbovu. Yuko wapi Nemanja Vidic wa 2008? Evra wa 2008? Pumzi imeisha kama gari bovu. Tactically United wataingia kwa nguvu kama ilivyozoeleka na kama umakini hautakuwepo wataadhibiwa kwa counter attack. Mchezaji wa mechi hii kwa upande wa United atakuwa Wayne Rooney.

    Mwisho

    Sioni Arsenal yenye kumzuia United kupata goli na naona kuna United yenye kumzuia Arsenal kupata goli endapo mategemeo makubwa yatakuwa kwa Mesút Ozìl.

    My prediction.
    ARSENAL 1 MAN UNITED 3
    **huu ni utabiri wangu mimi kama mimi na wala sio sheria. Tukutane 10:45pm**

    ReplyDelete
  2. Arsenal 3 Man U 1........man of the match ni OG

    ReplyDelete
  3. haya mpira umeisha bila magoli nini maoni yenu

    ReplyDelete

Powered by Blogger.