LIGI KUU ENGLAND ~ ARSENAL YAENDELEZA UTEJA KWA UNITED WAKATI LIVERPOOL WAKIFANYA YAO KIMYA KIMYA
Kwa miaka ya hivi karibuni Ushindi wa Arsenal kwa Man United umekua ni sare na hilo limethibitika baada ya kutoa sare ya 0-0 katika mchezo wa Ligi kuu England uliopigwa katika uwanja wa Emirates.
Mara ya mwisho Arsenal kuifunga United ilikua mwaka 2011 mwezi Mei na tangu kipindi hicho United imekua ikiionea Arsenal katika michezo wanayokutana.
Katika Mchezo huu Arsenal itabidi wajilaumu wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi za wazi baada ya mshambuliaji wake Olivier Giroud kushindwa kuweka mipira kimiani huku kipa wa United David De Gea naye akiibuka shujaa baada ya kuokoa michomo mingi ya washambuliaji wa Arsenal.
Man United wenyewe waliingia na hofu iliyoonekana kwa wachezaji wake lakini walijitaidi kurudi mchezo na kufanya mashambulizi ya kushitukiza ambayo nusu yazae matunda kama si juhudi za Kipa wa Arsenal Sczney na mabeki kama Laurent Koscienly na Per Metasacker. Maka mwisho wa mchezo Arsenal magoli yalikua 0-0.Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki katika nafasi ya pili wakiwa na alama 56 huku United ikibaki katika nafasi ya 7 wakiwa na point 42.
Katika mchezo mwingine uliopigwa katika uwanja wa Fulham ulishuhudiwa Liverpool wakirudi katika harakati za ubingwa baada ya kuibamiza Fulham bao 3-2 magoli ya Liverpool yakifungwa na Daniel Sturadge, Coutinho na nahodha Steven Gerard matokeo ambayo yanaifanya Liverpool kupanda katika msimamo kimya kimya huku wakiwa katika kiwango bora kabisa ambapo sasa wamefikisha pointi 53 katika nafasi ya 4.
Katika Uwanja wa St.James Park Wenyeji Newcastle walibaki midomo wazi baada ya kunyukwa na Totenham bao 4-0 magoli ya Spurs yakifungwa na Emmanuel Adebayor aliyefunga magoli mawili,Paulinho na Chadli na kuifanya Spurs kufikisha pointi 50 hivyo kuongeza idadi ya Timu zilizo na pointi zaidi ya 50 kufikia 5 hivyo kuongeza ugumu kujua timu ipi itanyakua ubingwa.
![]() |
| MSIMAMO - EPL |
Mechi zilizoahirishwa ni Everton v Crystal Palace na Ile ya Man City v Sunderland ambazo zitapangiwa tarehe nyingine.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


No comments