KOMBE LA FA ENGLAND ~ ARSENAL YALIPIZA KISASI KWA LIVERPOOL SASA KUKUTANA NA EVERTON ROBO FAINALI.



Ni wiki tu imepita tangu Arsenal walipopata kipigo cha 5-0 kutoka kwa Liverpool na leo ilikua muda muafaka kulipiza kisasi na kazi hiyo ilifanikiwa baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 lakini safari hii ikiwa katika kombe la FA.

Kama kawaida kwa Arsene Wenger aliweza kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ili kuwapa nafasi wengine pia mawazo yake yakiwa katika mchezo mgumu wa ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.katikati ya wiki.

Magoli ya Arsenal yalifungwa na Ox-Lade Chembalain na Lucas Podoski wakati lile la Liverpool likifungwa na Nahodha Steven Gerard kwa penati.
Sifa kubwa ziende kwa kipa wa Arsenal Lucas Fabianski ambaye aliokoa michomo mingi ya wazi ambayo ilikua ikipigwa na washambuliaji wa Liverpool Suarez na Sturadge.

Kwa matokeo hayo sasa Arsenal watakutana na Everton katika hatua ya Robo fainali baada ya Everton kuifunga Swansea 3-1 katika mchezo mwingine uliopigwa siku ya Jana.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo Wigan Athletic watasafiri mpaka uwanja wa Etihadi kuikabili Manchester City hivyo kukumbushia fainali ya kombe hilo mwaka jana.

Sheffield United baada ya kuifunga Nottigham Forest wao watasubiri mshindi kati ya Sheffield Wednesday au Chalton na wengi wanasubiri hapa pengine ikatokea mechi ya wapinzani wa jadi wa mji wa Sheffield.

Sunderland ambao tayari wameshafika fainali ya kombe la Capital one wao watasafiri kuikabili moja kati ya timu za Hull City au Brighton.

RATIBA KAMILI YA ROBO FAINALI

Arsenal v Everton

Brighton & Hove Albion or Hull City v Sunderland

Sheffield United v Sheffield Wednesday or Charlton Athletic

Manchester City v Wigan Athletic

.... Mechi za hatua ya Robo fainali zitapigwa tarehe 8-9 mwezi Machi mwaka huu.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.