LIGI YA MABINGWA ULAYA ~ MAN CITY NA BARCELONA PENGINE DUNIA IKASIMAMA KWA MUDA
Pengine leo inaweza ikawa siku nyingine ambayo dunia itabidi "Isimame" kwa muda kupisha mechi hii ambayo miaka ya zamani ingeweza kuonekana kama mechi rahisi ya upande mmoja tu na hata wengi wangesema Barcelona wamepata mteremko.
Ila hali ni tofauti kwa sasa kwan ukitaja timu bora duniani huwezi kuisahau Manchester City. Mafanikio ya machester City yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na Uwekezaji uliofanywa na familia ya kifalme ya Umoja wa nchi za Kiarabu.
Manchester City itaingia katika mtanange huo wa hatua ya 16 bora ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kujaribu kufanya hivyo mara mbili mfululizo katika misimu miwili iliyopita wakati huo ikiwa chini ya Roberto Mancini.
Ila itamkosa mpachika mabao wake Sergio Aguero ambaye yuko majeruhi Aguero ni amefunga magoli 26 katika mechi 25 alizocheza msimu huu katika mashindano yote huku wengi walitegemea angetoa upinzani mkali kwa beki ya Barcelona lakini faraja imekuja baada ya Samir Nasri na Fernandihno ambao wote walikua wagonjwa kurudi kikosini.
Machester City ndo timu pekee kutoka Ulaya iliyofunga magoli mengi msimu huu kwani mpaka sasa wameshafunga magoli 68 katika michezo 25 ya ligi kuu Nchini England ikifunga magoli 117 katika mshindano yote
Kwa upande wao Barcelona ndo wanaongoza ligi kuu Spain wakiwa wamefunga magoli 69 katika ligi msimu huu huku Neymar akirudi kikosini baada ya kuwa majeruhi.
Mechi hii pia itaikutanisha Barcelona na Yaya Toure ambaye alikua mchezaji muhimu katika mafanikio ya Barcelona katika utawala wa kocha Ridjkaard na Pep Guadiola. Uzuri wa mechi hii utakua kwa vikosi vyote kuwa na wachezaji wengi wa Spain.
Mechi hii itaanza muda mfupi ujao
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


No comments