LIGI KUU ENGLAND ~ HALI BADO TETE KWA BINGWA MTETEZI MAN UNITED

Goli la haraka kabisa la kipindi cha kwanza kutoka kwa mchezaji na nahodha wa Fulham Steve Sidwell liliweza kuwakatisha tamaa Man United ambao mpaka mapumziko walishakubali hilo goli,
Kipindi cha Pili kilishuhudiwa kazi kubwa ikifanywa na Benchi la ufundi kwa kuingiza washambuliaji wengine ili kujaribu kupenya ngome ngumu ya Fulham iliyokua ikiongozwa na John Heitinga.

Ilibidi United kusubiri mpaka dakika ya 78 kupata bao la kusawazisha na kuuvunja ukuta huo mgumu wa  bao lililofungwa na Robin Van Perse baada ya kuunganisha pasi ya Juan Mata.
Baada ya dakika 2 Michael Carick aliongeza goli la Pili kwa United na kufanya kuwa mbele kwa goli 2-1.
Wengi wakitaraji mchezo umeisha hasa pale zilipoongezwa dakika za nyongeza 5 ndipo maajabu yakajitokeza kwani Darren Bent alifunga goli la pili kwa Fulham dakika ya mwisho wa zile dakika  za mwamuzi ambazo zilikua 5.

MCHEZO WENYEWE

Man United ni dhahiri walihitaji ushindi huku wakiwachezesha nyota wake wote wakaja kukukutana na Fulham ambao point 1 tu kwao ni muhimu sana.
Kwa kifupi mchezo wote ulitawaliwa na Man United wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga huku pasi zilizolenga goli zikiwa ni 9 tu kwa upande wa United wakati Fulham wao walipiga mashuti matatu tu.
Man United walipiga jumla ya  mashuti 31 dimbani huku Fulham wakipia mashuti 6 tu mpaka mwisho wa mchezo.


:::::: MATOKEO MENGINE WEEKEND HII
  1. Liverpool 0-2 Arsenal
  2. Sunderland 0-2 Hull City
  3. Chelsea 3-0 Newcastle
  4. Swansea 3-0 Cardiff
  5. Norwich 0-0 Man City
  6. Aston Villa 0-2 West Ham United
  7. Crystal Palace 3-1 West Brom
  8. Southampton 2-2 Stoke City
  9. Totenham 1-0 Everton.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.