AJALI YA MUNICH ILIKUA PIGO KWA MAN UNITED
Leo Ni miaka 56 Tangu ajali ya Munich iliyohusisha klabu ya Manchester United ilipotokea katika jiji la Munich huko Ujerumani.
Ni ajali mbaya kuwahi kutokea machoni pa Wapenda soka duniani kote.
Tarehe 6 February 1958 katika Jiji la Munich yani Tarehe kama ya leo mwaka 1958
Ndege iliyokua imebeba kikosi cha Timu ya soka ya Manchester united ya England ikiwa na wachezaji wengi vijana waliokua wakinolewa na Kocha Matt Busby ambao walijulikana kama "Busby Babes" (watoto wa Busby ) kutokana na wastani wa umri wao mdogo kilikuwa kinasafiri kutoka Yugoslavia ambapo walitoka kucheza dhidi ya timu ya Red Star Belgrade ya nchini humo katika kombe la Ubingwa wa Ulaya wakati huo (European Cup)
Wakati wametua Ujerumani kuongeza mafuta katika uwanja wa ndege wa Riem jijini Munich, na baadae waendelee na safari ndipo ndege ikagoma kupaa katika ardhi iliyojaa barafu na Rubani alijaribu mara mbili bila mafanikio kwa bahati mbaya wakati Rubani akijaribu mara ya tatu ndipo ndege hiyo iliteleza katika njia ya kurukia ikapelekea kugonga uzio wa uwanja na ndege kuanguka katika baadhi ya majengo ya uwanja huo na kuwaka moto.
Juhudi za kuokoa maisha ya watu 44 waliokua katika ndege hiyo zilifanyika na bahati mbaya watu 20 wakiwemo wachezaji,maofisa wa timu,waandishi wa habari na baadhi ya mashabiki waliosafiri na timu hiyo walikufa papo hapo huku watu wengine wakikimbizwa hospitali ya karibu ya Recht De Isar akiwemo kocha Mkuu Matt Busby aliyekua Mahututi baadae taarifa zikatoka na kuripoti kuwa watu watatu zaidi walifariki na kupelekea wachezaji 8 wa kikosi cha kwanza kufariki dunia katika ajali hiyo.
MANCHESTER UNITED BAADA YA AJALI YA MUNICH
Wakati ajali ikitokea Man United ilikua ikishindana kuchukua ubingwa wa ligi msimu huo ikiwa imezidiwa pointi 6 na aliyekua aikongoza klabu ya Wolves.
Ajali hiyo ilimfanya kocha mkuu Matt Busby kutumia muda mwingi akiwa majeruhi kwani alikaa Hospital takribani miezi miwili na alipotoka alikataa kabisa kurudi kufundisha na hivyo United ikawabidi kumpa timu aliyekua kocha msaidizi wa Busby Jimmy Murphy ambaye wakati ajali inatokea alikuaWales akiinoma timu ya Taifa ya Wales.
United iliwatumia wachezaji wake waliokua katika kikosi cha akiba pamoja na wale waliokuwa katika kikosi cha Vijana huku ikifanya pia usaji kujiimarisha mchezaji kama Ernie Taylor aliyesajiliwa kutoka Black pool baadae wakamchukua Stan Crowtha toka Aston Villa. Pia walisajiliwa kwa mkopo wachezaji watatu toka timu ya mtaani ya Bishop Auckland ambao ni Derek Lewin,Bob Hardisty na Warren Bradley.
Hali ilikua mbaya zaidi baada ya kupoteza michezo yote 14 iliyobaki katika ligi huku timu ikimaliza katika nafasi ya 9 mwishoni mwa msimu na ndipo kocha Matty Busby aliporudi na kutengeneza kizazi kingine ambapo hapo ndo walipatikana nyota kama George Best na Denis Law
Baada ya miaka 10 kikosi hicho kilifanikiwa kushinda ubingwa wa Ulaya.
Kwa ufupi hii ndiyo habari kwa ufupi kuhusu Ajali ya Munich
Imetayarishwa na Edo Daniel Chibo
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments