MIWANI PANA YA EDO ~ YANGA NA MBEYA CITY LEO HAPATOSHI TAIFA

YANGA

Miaka ya zamani mechi kama hii ilionekana ni mechi ndogo kabisa kwa Yanga wakiamini itapata matokeo mazuri lakini msimu huu mambo yamebadilika na kadri siku zinavyoenda ndivyo tunaweza kupata timu zinazoweza kuleta ushindani.


MBEYA CITY
Azam Fc ni kati ya timu zilizokuja kuleta upinzani wa kweli katika ligi ingawa sasa kujitokeza kwa Mbeya City kumeleta changamoto mpya katika soka letu japo wengi wanajiuliza kama nguvu hii ni ya "soda" au nguvu halisi.

Katika uwanja wa Taifa Leo Yanga itaikaribisha Mbeya City ambayo imepanda daraja msimu huu huku Yanga wakiwa mabingwa watetezi na wakikamata nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 32.

Yanga imecheza mechi 15 Imeshinda mechi 9, ikitoka sare mara 5 na kupoteza mchezo mmoja huku wakiwa wamefunga magoli 33 na kufungwa magoli 12.
Mbeya City wao wamecheza mechi 15 wakishinda mechi 8 wametoa sare mara 7 na haijafungwa mchezo wowote mpaka sasa wakiwa wamefunga magoli 21 na kufungwa magoli 11 tu mpaka sasa.

HISTORIA INASEMAJE KUHUSU TIMU HIZI
  • Yanga na Mbeya City zimekutana mara moja tu katika historia ikiwa ni msimu huu wa ligi hatua ya kwanza katika mchezo uliopigwa katika jiji la Mbeya ambapo mchezo uliisha kwa sare ya 1-1.
  • Mbeya City na Azam FC ndiyo timu pekee ambazo mpaka sasa hazijapoteza mchezo wowote.
  • Tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania  Bara Mbeya City na Yanga zote zimeshapata pointi 4 kila moja yani wamecheza mechi 2 wakishinda moja na kutoa sare moja.
  • Mechi zilizopita Yanga walitoa sare ya 0-0 na Coastal Union wakati Mbeya City walitoka sare ya 1-1 na Ruvu shooting
Je Timu Gani itacheka leo?

Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 

No comments

Powered by Blogger.